Kiwewe kizito chawakumba walioshiriki au kushirikishwa katika jaribio la kigaidi la kumuua Mh. Tundu Antiphas Lissu!

Acha kutukana babu au ndio albadiri ndio imeanza kufanya kazi,ww kama hauusiki kaa utulie sio kutuletea povu lako hapa
 
Hahahah...yule wa 5000 kilo ya sukari !!
 
Bunduki ni nguvu za Giza? maajabu ya leo haya... acheni viroba akili zenu zirejee... Hoja yangu inatakiwa ijibiwe na hoja sio viroja!
Hebu nawe joingeze kidogo. Roho ya kutamani kuua sio roho ya kishetani? Kutamani fulani afe ili kutimiza malengo yako ovu ya kutokosolewa ni akili ya kishetani, giza na kuzimu.
 
Hebu nawe joingeze kidogo. Roho ya kutamani kuua sio roho ya kishetani? Kutamani fulani afe ili kutimiza malengo yako ovu ya kutokosolewa ni akili ya kishetani, giza na kuzimu.
Na si hivyo tu, kukalia hela zilizochangwa kusaidia matibabu ukisubiri majeruhi afe nadhani ni zaidi ya ushetani na laana yake inaweza kutafuna hadi kizazi cha tano. Yaani watu wengine hata hawaeleweki, kwa nini uutafutie ukoo wako laana hivi hivi ukiwa macho?
 
Laana yaendelea kushika kazi, hawajui washike lipi, leo wanasema hivi kesho wanasema vile na hawana tofauti na mfa maji...wanatapatapa, kila wanachokamata kinateleza na muda si mrefu wataanza kutajana moja baada ya mwingine. Bunge, Benki Kuu, Wizara, Serikali, Polisi...kila moja lwake, kiwewe kizito kimewakumba waliopanga, kuratibu, kusimamia na kutekeleza jaribio la kigaidi la kumtoa uhai Mh. Tundu Antiphas Lissu.
 
Mh!!!??? ... Huyu tayari Halal Badr imeshaingia kichwani jamani ... mlio karibu nae andaeni kamba ...

Sasa hivi anatorokea jalalani ... maana haya matusi sio dalili njema ... huyu tayari jamani ...
 
Mara ... ana Bima yake ... mara ooh familia iandike barua ... hawaeleweki ...
Hakuna mtu ambaye nafsi yake inamsuta na kumtesa kama Spika wa Bunge Job Ndugai...haraka haraka alikuwa wa kwanza kuwataka Wabunge wachangie matibabu ya Mh. Tundu Lissu lakini kuwakilisha michango hiyo ikawa shiiida, je alikuwa akisubiri nini?

Akakurupuka tena akidai Mbunge wa CCM ndiye alilipa gharama ya ndege iliyomsafirisha Mh. Tundu Lissu hadi Nairobi kwa matibabu. Je nyakati zote hizo hakujua Mh. Tundu Lissu ana bima? Hakujua kwamba bunge liliwajibika kutoa gharama za matibabu?

Huyu ni mfano moja tu katika waliokumbwa na kiwewe kizito wanavyoteseka lakini angalau yeye anatapatapa bado. Wapo waliopigwa butwaa hadi hata kauli zimewakwama, wapo kama hawapo wakishindwa hata kuifariji familia ya Mh. Tundu Antiphas Lissu.

Wengine hata kwa wanayoyatamka kwenye mikutano ya hadhara utadhani wamechanganyikiwa kabisa na wataendelea kuteseka kwa maovu waliyoyapanga hadi wakome. Mungu wa Rehema kaamua kuwashughulikia baada ya maelfu ya wananchi kukesha wakiomba.
 
Babako ndio anatakiwa amuuliza Kaini labda alimkuta enzi zake. au unamaanisha Kane wa Mieleka na yule Mchezaji mpira Uingereza?
Ninamaanisha Kaini yule muuaji mwenzenu; halafu mazwazwa wote hupenda kuwatukana watu wasikuwa na makosa nao!!! Babangu ana uhusiano gani na mjadala huu?
 
Ninamaanisha Kaini yule muuaji mwenzenu; halafu mazwazwa wote hupenda kuwatukana watu wasikuwa na makosa nao!!! Babangu ana uhusiano gani na mjadala huu?
Sasa kama unamkinga babako cain umri wake babako anaingia mara ngapi? au unamdharau sababu humjui na why ulimleta kwenye mjadara? Mimi nakupa majibu ili utulie na akili yako ipanuke maana imelala.
 
Itakuwa unauhusiano wa karibu na gurudumu sio bure
 
Unaweweseka sana mpaka unatia huruma!
 
Magufuli ana Mungu! Mamlaka yake haipo kwa bahati mbaya na yote mnayoyaongea ni ya kufikirika tu hakuna aliyehakikisha upopo unaomwagwa humu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…