Kizazi cha ndugu zetu Albino Kitakuwa wapi mwaka 2012?

Kizazi cha ndugu zetu Albino Kitakuwa wapi mwaka 2012?

Shadow

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2008
Posts
2,897
Reaction score
675
Kutokana na baadhi ya waendesha nchi kuamua kuweka pamba masikioni kuhusu suala hili la mwendo kasi wa mauaji ya ndugu zetu, watanzania wenzetu wenye ulemavu wa ngozi maalbino.

Piga picha kwa hali hii ilivyo hivi sasa, je hiki kizazi cha ndugu zetu hawa kitakuwa wapi mwaka 2012?

Tafakari, chukua hatua.

Shadow.
 
Hatua ni kuwa, wale wanaoua albinos nao wauawa bila kufikishwa mahakamani.......kwa maneno mengine, wananchi wadili na hawa wauaji kama wanavyodili na vibaka!! SIMPO!

Mzee your nameis mine, Heshima yako mzee:

Asante kwa mchango wako mzuri, napenda nichepuke kidogo kutoka katika msimamo wako. Kuchukua sheria si suluhisho, refer kwenye vita ya kuwachoma vibaka na sasa kuwawamba msalabani lakini ubakaji hupo palepale kwa sababu ya kasoro nyingi katika jamii yetu mfano mipango mibovu ya kumwandaa kijina kujitegemea baada ya kumaliza shule, job creation ni kama sifuri. Mwungwana anaweza kutuelezea kuhusu ajira milioni moja.

Suala je, hawa ndugu zetu watasalimika mpaka mwaka 2012 kama mwendo huu wa kuwaangamiza utaendelea? Je jamii ifanye nini pale inapoonekana waendesha nchi wako kwenye usingizi wa pono katika kutafuta suluhisho na kuzuia haya mauaji? Tatizo lipo wapi? Social Engineers wa Tanzania mnaweza kutusaidia. Maana hata kama leo tutapitisha sheria kali bila ya kutambua wapi tatizo lipo ni kazi bure.
 
Back
Top Bottom