Morning_star
JF-Expert Member
- Apr 21, 2018
- 6,042
- 17,320
Nilikuwa nafuatilia kwa ufupi baadhi ya viongozi na umri wao wa kuanza kubeba majukumu ya kitaifa nikagundua walikuwa na umri mkubwa.
Kwa mfano: Juliasi. K. Nyerere alianza darasa la kwanza akiwa na umri wa miaka 12. Na woote viongozi wa kizazi chake walianza shule kwa umri huo.
Rashid Kawawa, alianza shule akiwa na umri wa miaka 10 na wote wa kizazi chake ni katika umri huo.
John Magufuli, alianza shule na miaka 8 na wote wa umri huo. Sasa hivi kizazi tulichonacho kinaanza shule na miaka kuanzia 4 hadi 6 na wengine kumaliza chuo hama kabla hawajatimiza miaka 18 au miaka 18 inawakuta wakiwa chuo.
Mimi nadhani kama taifa tuna changamoto kubwa ya weredi wa uwajibikaji katika majukumu ya kaya, jamii hadi taifa!. Kuna mambo yanahitaji ukomavu wa akili na sio elimu ya darasani.
Nikirejea kwenye Biblia (Waebrania 5:14 "Lakini chakula kigumu ni cha watu wazima, ambao akili zao, kwa kutumiwa, zimezoezwa kupambanua mema na mabaya").
Tukija katika kuoa na kumudu majukumu ya familia kijana alikuwa anapewa mke kuanzia miaka 35. Sasa hivi mmomonyoko wa maadili na uhalifu na kuongezeka kwa changamoto za tamaa za kumiliki mali na vifo kabla ya wakati ni kutokana na rika la umri mdogo kulazimishwa na mfumo kubeba majukumu makubwa wakiwa watoto.
Nachukulia mfano mimi mwenyewe alafu nikiangalia watoto wangu kwa umri walionao na werevu wao nalinganisha na mimi nilikuwa na werevu gani, alafu nalinganisha na viwango vya elimu walivyonavyo sasa na werevu wao nikilinganisha na kipindi hicho na mimi nilikuwa na werevu hupi.
Nikagundua tumechukulia elimu ya darasani tukadhani inaweza kubeba majukumu ya maisha nikaona tumefeli sana.
Kwa ufupi tuna kizazi chenye elimu lakini hakina maarifa! Migogoro ya kazini, ndoa, utii wa sheria n.k vinasababishwa na kuchukulia watoto kama ni watu wazima kumbe wanatakiwa kuwa chini ya uangalizi.
Changamoto imekuwa ni uwezo wa kifedha na dharau kwasababu heti fedha ni kipimo cha akili kumbe sio!
Mimi nilianza shule nikiwa na miaka 12. Nilioa nikiwa na miaka 35 na kupata mtoto wa kwanza nikiwa na miaka 36. Nimepata akili za kumiliki nyumba (kihalali) nikiwa na miaka 45. Niliacha kazi (kwa hiali kabisa) za kuajiriwa na kujiajiri nikiwa na miaka 48.
Katika mwingiliano wa vijana wa rika mbalimbali na mukutadha wa uongozi kitaifa na kimataifa nimejiridhisha kuwa tunafeli kwa kujiaminisha na kuamini watoto wanaweza kubeba majukumu ya kifamilia na kiuongozi!
Nimejaribu kufuautilia siasa za mataifa makubwa kama Marekani, hawakupi majukumu makubwa ya kitaifa mpaka wamejiridhisha uzoefu na UMRI wako kama vinalandana!
Kwa kizazi tulichonacho, naomba watunga sera ebu watusaidie kupitia upya umri, uzoefu viendane na majukumu tunayowapa.