Kiziwi anafikiri kwa kutumia lugha gani?

Kiziwi anafikiri kwa kutumia lugha gani?

superstar1

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2014
Posts
222
Reaction score
176
Hivi, eti mtu ambaye ni kiziwi toka alipozaliwa huwa anafikiri kwa kutumia lugha gani jamani?
 
Utaanza kuuliza na kipofu wa kuzaliwa kwenye mawazo yake huwa anaona nini
 
kwa ubongo!
as usual something blind bind in ur mind make it kind!!
 
Hivi, eti mtu ambaye ni kiziwi toka alipozaliwa huwa anafikiri kwa kutumia lugha gani jamani?

Hivi wewe nami twafikiria kwa lugha gani? Na yeyote asije kudangaya eti wewe hufikiria kwa lugha ya Kiswahili...Mtoto wa miezi sita hufikiria kwa lugha gani? Kwanini anapobebwa na mtu fulani anaanza kulia? Kwanini akimwona mtoto mwingine naye anabadilika?
 
Jaman mtoa mada mnaweza kumwona katoa mada pumba, ila jaribuni kufikiria mara mbilimbili, moja ya function ya lugha ni kufikiria yaan imagination. Mfano unasema kesho niyaenda shuleni. Hapo umetumia lugha. Sasa kwa kiziwi wa kuzaliwa anatumia lugha gani? Mi nanona huu ni mjadala mzuri kwa kuongeza maariga na ujizi.
 
Kwani kufikiri ni lazima ufikiri kwa lugha? Mtoto mdogo anapozaliwa kabla ya kujua lugha huwa anafikiri vipi?

Usichanganye vitu viwili.

Huwezi kuwa na lugha bila fikra, lakini unaweza kuwa na fikra bila lugha.
 
Well written mkuu,

Zaidi, lugha yoyote ni matokeo ya fikra ila zinakuwa zimepangiliwa kikanuni...
 
Hivi, eti mtu ambaye ni kiziwi toka alipozaliwa huwa anafikiri kwa kutumia lugha gani jamani?

Kiziwi wa kuzaliwa katika kufikiria hufikiri kwa kutumia lugha za vitendo halisi kwa mfano kama anataka kuukumbuka mtaa wa zamani katika fikra zake atakumbuka majengo ya mtaa ule.
Au anahitaji chakula katika fikra zake atakumbuka sinia ya chakula fulani.
Kwa ufupi hafikiriii kwa kutumia kiswahili cha kuongea bali anavuta fikra za picha halisi za vitendo vyenyewe.
 
Back
Top Bottom