Kizungumkuti cha Maslahi katika Utumishi wa Umma

Kizungumkuti cha Maslahi katika Utumishi wa Umma

mliverpool

JF-Expert Member
Joined
Jan 6, 2015
Posts
1,565
Reaction score
2,944
Maisha ya utumishi yananiacha hoi sana ikifika muda wa maslahi na utofauti baina ya taasisi na taasisi!

1. Kuna taasisi mishahara yao ni ya kawaida kabisa ya scale ya msajili wa hazina, ila ukija ktk posho na madokezo kwa mwezi watu wanakunja hadi milion 3 , 4 hadi 5!bosi hakatai dokezo mradi tu jina lake likae juu kwanza,kila kazi unayofanya unaandikia dokezo na linapitishwa mradi wale wadau muhimu kuanzia mkurugenzi mkuu,mhasibu,cashier hadi mtu wa msjala anayeingiza na kutembeza dokezo awepo.

2. Kuna taasisi wana scale kubwa za mishahara mfano hadi milion 2 hadi kwa anayeanza ila maisha ndani yake ni magumu balaa,hakuna posho wala maslahi yoyote ukiacha mshahara mwezi mpaka mwezi bosi hata kulipa OT anaona unafilisi hela ya taasisi!

3. Kuna mabosi wanaroho mbaya maslahi yote ya kitengo au idara anakula yeye,safari zote bosi anaenda mwenyewe hata anazoweza kwenda ofisa wa kawaida tu.

4. Kuna maofisi kuna watu wanafaidi balaa wanapata maslahi yasiyo na mfano ila ndani ya ofisi hiyohiyo kuna watu wanalia njaa anatamani aondoke muda wowote! Chnzo ni makundi ya mabosi bosi/mkuu wa kitengo anakuwa na watu wachche anaokula nao.

5. Kuna vi taasisi ukiviangalia ni vidogo na majukumu yake ni madogo hazina watu wngi ukiiangalia kwa nje unaidharau ila wanalipana vzr mpaka unashangaa ukisikia stori zake, wanalipana posho mpaka zinamwagika na kuna mitaasisi mikubwa kila mtu anaitolea macho ila hamna kitu watu wake wanalia njaa balaa!
 
Iyo ipo tu mkuu hususan kwa wale wazee wa safari hapo mpaka uwe na connection la sivyo hupati ng'o wengin wabaguzi hata mpitie utumishi kwa interview bado moto wa maslahi kwa ndani utakutana nao

Wengin training inaandliwa kwa wote wanapa taarifa wachache kwa kigezo cha majukumu then kule wamesomba posho za watumishi wote wanalipa wachache zingine wanatia mfukoni

My take usifuatilie mambo ya kiofisi yatakuumiza kama unaona hauna stream kwa sie tusiopenda shobo fresh tu kikubwa unakula halali yako

Wengine unaweza kosa overtime wakapewa wengine ambao hawana majukumu wanakamilisha ratiba tu ili wasaini haya mambo ni balaa

Kingine usiwe na shobo mfano labda watu wameorodheshwa kwenda safau we haumo usiulize wala nne kikubwa mshahara unapata. Jitahidi kutafuta fursa za pembeni kama biashara

Kuna ofisi kuna matabaka ni hatar sana ukabila na udini humo watu wanatafutiana visa tu
 
Back
Top Bottom