Kizungumkuti cha NECTA wanafunzi hawa hawakufanya mtihani kidato cha IV lakini wamefaulu!

Kwa mujibu wa NECTA watahiniwa waliosajiliwa ni 203 mmoja matokeo yake yamekuwa withheld wanne hawakufanya mtihani ambao ni hawa (tofauti na Bwana Bujugo) 198 wako "clean"

[TABLE="width: 453"]
[TR]
[TD]S1197/0044[/TD]
[TD]F[/TD]
[TD]-[/TD]
[TD]ABS[/TD]
[TD]CIV-X HIST-X GEO-X KISW-X ENGL-X BIO-X B/MATH-X[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]S1197/0091[/TD]
[TD]M[/TD]
[TD]-[/TD]
[TD]ABS[/TD]
[TD]CIV-X HIST-X GEO-X KISW-X ENGL-X BIO-X B/MATH-X[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]S1197/0144[/TD]
[TD]M[/TD]
[TD]-[/TD]
[TD]ABS[/TD]
[TD]CIV-X HIST-X GEO-X KISW-X ENGL-X BIO-X B/MATH-X COMM-X B/KEEPING-X[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]S1197/0172[/TD]
[TD]M[/TD]
[TD]-[/TD]
[TD]ABS[/TD]
[TD]CIV-X HIST-X GEO-X KISW-X ENGL-X BIO-X B/MATH-X[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
Lakini mkuu aliyeibua kashfa hiyo ni mkurugenzi wa shule na namba na majina ya hao watoto anayo na itakua anawajua fika...kwa hiyo suala la namba kutumika kuleta utata halina mantiki yoyote hapa...
 

Kwa hiyo Bujugo kajichanganya? Maana naona Green Acres wamefeli sana. Sasa anahisi atakosa biashara ya shule yake. Anatafuta pa kutokea. Na Green Acres miaka ya nyuma walikuwa na tabia ya kuonyesha wanafunzi mitihani...!
 

Bujugo si mkuu wa shule, bali ni Mkurugenzi. Anamiliki shule kuanzia awali mpaka chuo.
Kuna namba ya mwanafunzi amesema hawakufanya masomo ya B/Keeping na Commerce lakini wamepewa alama. Baada ya kufuatilia nimegundua ya kwamba hiyo namba imepata FLD ya 34.
Kwa taarifa tu, Bujugo ni bonge la fisadi na tapeli wa kutupwa hapa DSM.
 
Lakini mkuu aliyeibua kashfa hiyo ni mkurugenzi wa shule na namba na majina ya hao watoto anayo na itakua anawajua fika...kwa hiyo suala la namba kutumika kuleta utata halina mantiki yoyote hapa...

Mkuu huyu jamaa kama angekuwa na uhakika na anacho kisema angekuwa ameisha chukua hatua stahiki kabla ya kukimbilia kwenye vyombo vya habari. Hii issue kama ni kweli ni very serious issue kama ningekuwa mimi ningehakikisha nimechukua hatua zinazotakiwa then nikija kuujulisha umma sisemi kwamba nadhani matokeo yamechakachuliwa bali naongea kwa uhakika sina imani na matokeo kabisa.


Ndugu yangu naomba nikujulishe kwamba wakurugenzi wa shule wengi ndio wamiliki wa shule sio watendaji (watendaji ni walimu wakuu), mara nyingi hawajui nini kina endelea au taratibu zikoje.

Kwa maoni yangu hii issue ni serious kama ina ukweli hivyo inatakiwa achukue hatua mapema badala ya kuleta porojo. Naomba mwandishi wa habari husika kwenye gazeti la Tanzania Daima wamfuate mkuu wa shule waka muulize mwalimu mkuu kuhusu uthibitisho wa kauli ya mkurugenzi wake na waombe nyaraka zozte za usajili wa wanafunzi walizopokea kutoka NECTA zenye majina na namba ili kuthibitisha kauli hiyo. Wakitoka kwa mwalimu mkuu wakamhoji Katibu Mtendaji wa NECTA kutoakana na kauli na uthibitisho wa walicho kipata kutoka huko shule husika. Vile vile wanaweza kuwatafuta wanafunzi husika wanaohusishwa suala na kuwa uliza walifanya mitihani kwa kutumia namba zipi?

Natuamaini kama mkurugenzi anajua ni hatua gani za kufuata ili kuwasaidia vijana wake na watanzania wengine kwa ujumla. Kwani kama hii issue imetokea Green Acres kuna uwezakano mkubwa imetokea na sehemu zingine hivyo achukue hatu kuinusuru nchi yetu.
 
Ndugu zangu wana jf, naamini kabisa kwamba dhamira hasa ya chombo hiki ni kutuweka pamoja na kuweza kusaidiana katika maswala mbalimbali yanayotuzunguuka kimaisha katika nchi yetu, ieleweke kwamba hii mitandao ya kijamii kama tutaitumia kwa hekima na busara, basi inaweza kuwa mojawapo ya njia kuu za maendeleo Kitaifa.

Nimesikitishwa na wana jf waliomjibu mtoa mada ya shule ya Green Acres, kwa kweli huku ni kukatishana tamaa, na kwa mtindo huu watu wengi wanaweza kuwa waoga katika kutoa maoni yao kuhusu maovu mbalimbali yanayoendea kufanyika. Ndio maana ikaitwa mitandao ya kijamii, yaani tongee, tushauriane, tuelekezane kindugu, yeye ameshatupatia taarifa mpaka pale alipofikia, sasa mwingine angeendeleza kwa kufuatilia kwa Mkurugenzi wa shule hatimaye ukweli ungepatikana bila bughudha lawama au kupondana.
 



Mwenye uwezo kubwa hebu fuatilia hizi threads:

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-elimu-education-forum/405324-necta-yatikiswa;-yacharuka.html

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...-wa-green-acres-secondary-school-aumbuka.html
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…