Mimi nashindwa kuamini hawa uvccm kama wanaelewa maana ya hii vita, hawa vijana wamelewa mvinyo ya damu za watanzania na hawajui kitu gani wanapigania, na nani wanampigania na adui ni yupi, anaefaidika ni nani! waziri kijana mwenzao (ngeleja) alitaja wamiliki hadharani,nakutuhakikishia kuwa atalipa pesa, sitta na mwakyembe wakasema haiwezekani kampuni hewa kulipwa pesa za watanzania kwa kampuni hii ya kisanii, ccm vijana nao wanatoa tamko lao kuwa hawaoni sababu ya bosi wao kulipa, huu ni ushaidi tosha ukijumlisha na ambao tumekuwa tukiupata tangu na kabla Lowassa kujiuzuru, kuwa NCHI INAENDESHWA NA WAKORA skendo hizi haziwezi kuisha bila rais kuwajibishwa ni dhahiri kuwa JK na wenzake wamedhamiria kutekeleza haya malipo. Chama chao kimetupa uhakika kila mara tena hadharani kuwa, nchi hii inaliwaje tena na nani, kama hilo halitoshi wadhalimu hawa wanajitahidi kututoa kwenye hoja asilia na kutupeleka kwenye propaganda za udini.
MAONI YANGU, huu ni wakati taifa(mwananchi) tunapaswa kumuwajibisha raisi na wasidizi wake, sababu hakuna kitengo au wizara ktk serikali hii waweza kukuta wizi, uporaji, unyang'anyi, udhalimu ambao hauitaji kuumiza kichwa kwa kufikiri kujua source ni Rais kikwete. wanao uliza kauli ya rais, tamko ama kuakaa kwake kimya! mnataka aseme nini wakati mnajua kabisa kwa uwezo manunuzi na ridhaa aliyopewa awamu ya kwanza,ambayo (naamini pia udhalimu ulifanyika kushinda) akapanga mikakati ya kuiba tena ili ashinde kwa udhalimu huu huu. Any way alijimilikisha urais, tena bila haya ya uso mbele ya watu wake na mataifa. Huyu mtu mnamuomba atoe tamko kwa nani, na la nini, aseme kitu gani! kwamba dowans si kampuni? ama siijui? sihusiki nayo, sijawahi isikia... au najua ninacho kifanya mniache, msiniingilie mamlaka yangu, lazima nilipe pesa za mshikaji, au watanzania walio wengi wako tayari kula nyasi lazima dowans ilipwe, nchi inaheshimu sheria za kimataifa sana nimekuwa waziri/mambo ya nje muda mrefu tunaaminika kwa kutii, au tuvumiliane tu nimalizie dili zangu niwaachie nchi yenu.
Mnataka hasa majibu gani kutoka kwa JK ambayo bado hamjayapata,hamyajui au hamjapewa........this dude is a criminal! he knows that, he is very familiar for his violation of laws and constutution, to which he claim to protect. huwezi kusema unaipenda sheria ya kimataifa kuliko sheria ya watu wako ambayo wewe mwenyewe umeikanyaga na kuidharau. ANGALIZO, Dont expect someone to respect you if you dont respect yourself. wananchi tumeshindwa kujieshimu tumewaruhusu politicians kutununua, kwa fedha,chakula, ulaghai, vyeo, madaraka, ajira, dhuluma, matokeo yake unapo kubali kuuza utu wako kwa hayo, hivyo si kazi yako tena kumpangia mnunuzi akufanyeje au akutumieje? thats non of your business............!!! for him you are a slave and he is the master! usitegemee kushirikishwa, kuombwa ushauri, kushiriki maamuzi, kuhoji,kufuata sheria, kulalamika, kugoma, kukataa,kufurahi, kuwahuru, uhakika wa maisha au kuishi siku nyingi kwa raha, laa! sifa na haki zako zote uliuza kwa kujua ama kutokujua thamani yake. kwako wewe haki yako ni rehema za bwana wako, na wala si uhodari wa kumsihi au kumuomba kutoa tamko kuhusu hali yako kwamba umechoka kiasi gani ama uko hoi kiasi gani,umezalisha kiasi gani na atumie kiasi gani. Lugha hiyo fisadi haijui wala hana shida ya kujifunza, kumbuka alivyokupata...........
NINI CHA KUFANYA, Mtumwa anapochoka NA MAANISHA yule aliyochoka kweli na ana dhamira ya kweli ya kuitaka haki yake aliyo uza au poteza si kwa kumuomba ama kum-please mnunuzi kwa sababu hatakurudishia kwa style hiyo na utangoja sana..... Tanzania, utangoja sana.
kuna wale walio pata rehema za mnunuzi na wanahisi hawaitaji kuitisha haki yao tena, wao wameridhika ingawa nao ni watumwa hata kama tunalingana hali ya machungu na makali ya utumwa. wao ni watiifu na hawako tayari kumsaliti bwana wao, tujitahidi kuwaelewesha kwamba tumechoka:frusty: tukovitani. vita hii sio ya RA ma JK tu kwani tunajua kuna kikundi ambacho kinampa nguvu ya kuchochea ushabiki wa ubadhirifu hao pia ni adui zetu. JF let we have the same aim and same objective, to find who ever against our war...... hawa ndio wanao turudisha nyuma. pili kumshinikiza na kumtaka JK kutoka madarakani... HOW.. BY ANY MEANS NECESSARY.