Viongozi wa nchi, fanyeni hima kuinusuru hali hii, msiwalipe Dowans-Richmond, mtawadhulumu watanzania. Someni alama za nyakati kuinusuru nchi, wananchi wameanza kuchoka na ubabaishaji, ufisadi na kubebanabebana. Yanayoendelea sasa si lengo la watanzania. Rekebisheni makosa, simameni imara yasijetokea ya Tunisia na Ivory Coast. Viongozi wetu kumbukeni kuwa tabia/mielekeo na mienendo ya binadamu ni ileile pale wanapochoshwa na hali fulani.Tusisubiri hadi watanzania wachoke na hali ya mambo, inabidi kusimama imara kutetea haki za watanzania na kukemea waziwazi vitendo vyote vya dhuluma,ufisadi,ugandamizaji,unyanyasaji na unyamazishwaji, Mkiikataa hali ya dhuluma tunayotaka kufanyiwa na hawa Dowans-richmond, Mtakuwa mmeukataa Ukoloni mamboleo. Mkiikubali hali hii, basi mtakuwa mmeukubali ukoloni mamboleo, na Uhuru wetu utakuwa umeingia dosari. Wala msitetee kuendelea kuwalipa,KATAENI, Mkikataa na Watanzania watawaunga mkono, ila mkikubaliana na dhuluma hii, Watanzania wataweka shaka na pengine kuwakataa ninyi na hao Dowans-richmond. MSISUBIRI HADI WATANZANIA WAKATAE, ENYI VIONGOZI WETU KATAENI SASA kwani wakati ni huu.