KKKT acheni Mfumo Dume

KKKT acheni Mfumo Dume

Alex Fredrick

JF-Expert Member
Joined
Jun 21, 2016
Posts
697
Reaction score
1,358
Miaka ya nyuma na udogo wangu nimekuwa nikiabudu KKKT Usharika wa Kariakoo.

Niliacha kuabudu KKKT mwaka 2008 nadhani kipindi hicho Kimaro ndo kapewa Usharika wa Kariakoo..

Niliondoka baada ya kuona Ibada zimekuwa za kawaida sana sio za kuongozwa na Roho kama Biblia inavyotaka.

Mwanzilishi wa KKKT Dr Martin Luther ambae ndiye baba wa Upentecostal kama angefufuka leo na kuona Dhehebu ambalo ameliasisi liko hivi nadhan angesikitika sana..

Kwa uzoefu wangu mdogo Kanisa la KKKT miaka ya hivi karibuni limepata shida hasa baada ya kupata Wachungaji wa Kiroho wenye maono tofauti na desturi ya hii Dini kongwe..

Mchungaji Eliona Kimaro, Mchungaji Willbroad Mastai na Mchungaji Ismael Mwipile wamekuwa chachu na hamasa kwa washarika tofauti na mazoea ya Ibada kuongozwa na Litulujia.

Mafarisayo na Masadukayo wamekuwa wakiwaona hawa Wachungaji kama mwiba wenye lengo la kuaribu"Ugali" wao..

Martin Luther alikataa mafundisho ya Dini au ya kibinadamu na ndio sababu ya kuanzisha KKKT lengo Kanisa liongozwe kwa msaada wa Roho(Yohana 4:24..Matendo 2.37 na 39..

Dr Eliona Kimaro na wenzie ambao naamini siku zao zaja wamekuwa wanazuoni mahiri wa muasisi wa KKKT Martin Luther tofauti na Mafarisayo na Masadukayo.. Wafia Dini.

Kinachotekea leo ni Mfume Dume ndani ya Kanisa hili kongwe Duniani tofauti na kile alichopigania muasisi wake Dr Martini Luther

Ushauri wangu kwa Kanisa hili viongozi wakubali kubadilika na kukosolewa pia Ibada ziongozwe kwa msaada wa Roho na sio Litulujia

Mwisho kwa KKKT :Mchungaji Kimaro, Mchungaji Mastai, Mchungaji Mwipile. Kioo Tuelekeacho..

Alex
 
Dini na makanisa yote yali anzishwa kwa maslahi ya wanadamu.

Mungu hana kanisa wala dini....
 
Watu wanajiandaa kwa uchaguzi, vijana tishio lazima watishwe.
 
Ivi na lile swala la kurejeshwa kundini nalo limekaaje ?.
 
Back
Top Bottom