KKKT : Maaskofu hatujagawanyika kuhusu Katiba

KKKT : Maaskofu hatujagawanyika kuhusu Katiba

Greenwhich

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
1,337
Reaction score
968
Askofu Benson Bagonza wa KKKT Dayosisi ya Karagwe amepinga vikali kauli ya serikali kwamba maaskofu wamegawanyika kuhusu Kura ya Hapana kwenye Katiba Mpya.

Askofu Bagonza ambaye ni mjumbe wa CCT ameonya kauli ya Samwel Sitta kwamba Serikali haitarudi nyuma kuhusu katiba mpya.

Askofu Bagonza ambaye ana msimamo thabiti amesema wapo maaskofu wa mfukoni wanaoandaliwa na Serikali ambao wanatumika kujibu hoja mbalimbali za kanisa.

Akizungumzia Kauli ya Kadinali Pengo kupingana na maaskofu wenzake, Askofu Bagonza amesema huo ni msimamo binafsi wa Kadinali Pengo na siyo msimamo wa Kanisa Katoliki nchini.

Askofu Bagonza amesema msimamo wa Kanisa Katoliki nchini unatolewa na TEC ambalo ni Baraza la Maaskofu Katoliki nchini.

Askofu Bagonza amesisitiza kwamba pamoja na msimamo binafsi wa Kadinali Pengo lakini ameruhusu Tamko la Maaskofu kusomwa katika Makanisa yote ya Jimbo lake la DSM.

Askofu Bagonza ameishangaa serikali kusema Kanisa halina haki ya kuwataka waumini kupiga kura ya Hapana.

Askofu Bagonza amesema.." Kama CCM na serikali yake wanawashawishi watu wapige kura ya Ndiyo, Ukawa wamewaeleza watu wao wasusie,iweje iwe tatizo kwa Jukwaa la Wakristo kuwaeleza wafuasi wao wapige kura ya Hapana?"...alihoji.
======================

Dar es Salaam. Mjadala kuhusu tamko la Jukwaa la Wakristo Tanzania umezidi kupamba moto baada ya Askofu Benson Bagonza wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzani (KKKT) Dayosisi ya Karagwe, kupinga kuwapo kwa mgawanyiko miongoni mwao kama unavyosemwa na Serikali.

Kauli ya Askofu Bagonza imekuja siku moja baada ya Serikali kupitia Waziri wa Uchukuzi anayekaimu nafasi ya Kiongozi wa Serikali bungeni, Samuel Sitta kueleza kuwa maaskofu wamegawanyika na mgawanyiko huo hauwezi kubadili msimamo wa Serikali.

Sitta, ambaye pia alikuwa mwenyekiti wa Bunge Maalumu, alisema maaskofu hao wawaache wananchi waamue wenyewe aina ya kura wanayotaka kuipigia Katiba Inayopendekezwa.

Akizungumza na gazeti hili jana, Askofu Bagonza alisema hakuna mgawanyiko na Serikali imeandaa maaskofu wake mfukoni ambao huwatumia kujibu hoja mbalimbali za maaskofu.

Alitoa mfano wa askofu mmoja ambaye alisema hafahamiki kwa Kanisa la Pentekoste, Walutheri wala Wakatoliki.

Kauli ya Pengo

Akizungumzia kauli aliyotoa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo inayopingana na maoni ya Jukwaa la Wakristo Tanzania, Askofu Bagonza alisema hayo ni maoni yake binafsi na haiwezi kuwa sauti ya Wakatoliki wa Tanzania.

Askofu Bagonza alisema sauti ya Wakatoliki hutolewa na Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) ambalo ndilo mwanachama wa Jukwaa la Wakristo Tanzania.

"Mwadhama yeye ni mjumbe wa TEC, alitoa tu maoni yake na aliagiza tamko letu la jukwaa lisomwe kwenye makanisa ya jimbo lake la Dar es Salaam," alisema Askofu Bagonza na kufafanua kuwa tamko lililotolewa na jukwaa ndiyo kauli rasmi ya Wakristo.

Askofu huyo alisema kabla ya msimamo wa jukwaa hilo kutolewa, siku tatu kabla TEC ambayo Kardinali Pengo ni mjumbe, lilitoa tamko lenye ujumbe unaofanana na wa jukwaa, ukiitaka Serikali kuahirisha kura ya maoni la sivyo waumini wahamasishwe kuipigia kura ya hapana Katiba Inayopendekezwa.

Msimamo wa makundi

Askofu Bagonza alisema suala la Katiba ni la Watanzania wote, hivyo makundi katika jamii yana haki ya kutoa maoni yake yanayoweza kutofautiana na ya wengine.

"Kama CCM na Serikali yake wanashawishi watu wapige kura ya Ndiyo, Ukawa wamewaeleza watu wao wasusie, iweje iwe tatizo kwa Jukwaa la Wakristo kuwaeleza wafuasi wao wapige kura ya Hapana?" alihoji.

Hata hivyo, Askofu Bagonza alisema jukwaa katika mjadala wake halikujikita katika mambo yaliyomo katika Katiba Inayopendekezwa, bali yale yaliyoachwa na jinsi mchakato ulivyokwenda.

Mahakama ya Kadhi


Kuhusu Mahakama ya Kadhi, Askofu huyo alisema jukwaa hilo halina tatizo na uzuri au ubaya wa mahakama hiyo, bali Serikali kujihusisha na suala hilo na kuifanya kama ahadi ya kuwavutia Waislamu kuipitisha Katiba Inayopendekezwa katika Bunge la Katiba.

Chanzo:
Mwananchi
 
Asante sana Askofu Wangu.....

Naomba askofu Wangu wa Dayosisi Ya Kaskazini na Wewe uuunge mkono Kura ya HAPANA.....hii katiba sio chaguo la wananchi.....

Huyu Askofu ni Nabii wa ukweli kama alivyo Severine Niwemugizi
 
Kardinali Pengo alisema hivi;
Pamoja na tafakari nzuri kabisa na mawazo makini yaliyotolewa katika barua hizi, kufikia hatua ya kumwambia kila mkristo katika lile tamko la jukwaa la wakristu kusema itakapofika siku ya kupiga kura kuhusu mapendekezo ya katiba twende kwa moyo mmoja na kila mmoja apige kura ya hapana, sijui kwa kiasi gani tunaheshimu dhamiri za waumini wetu.

Kuwaambia sisi kama maaskofu tunasema mwende mkapige kura ya hapana. Na kwanini tuwafanye hivyo waamini wetu, tuwageuzi ni watoto wadogo ambao lazima kuwaambia lazima mwende mkapige kura ya hapana. Hilo ni jambo ambalo linadhalilisha uhuru wa wana wa Mungu ndani ya waamini wetu.

Hatuna uwezo wala hatuna haki ya kuwaambie mwende mkapige kura, lakini kura hiyo iwe ya hapana. Na kwanini hiyo hivyo, je waamini wetu ni watoto wadogo wasioweza kufikiri na kutafakari wenyewe kiasi kwamba tuwaambie nendeni mkapige kura ya hapana. Tumepata wapi haki hiyo, tumeipata wapi haki hiyo? Hilo ni swali muhimu sana.

Kwa matamko haya mawili narudia tena kusema, pamoja na umakini wake lengo au tukio la mwisho ni kwamba linagawa taifa lete kati ya wakristu na wasiokuwa wakristu. Matokeo yake tunaweza kuyafikiria sisi wenyewe. Vile vile linagawa wakristu kutoka kwa serikali yao jambo ambalo kwa kweli haliwezekani.

Ndani ya serikali yetu ya Tanzania katika uonogozi wake wapo waumini wetu wakatoliki na wako waamini wakristo ambao ukisimama na kuwaambia serikali au kanisa linasimama dhidi ya kanisa ni kuwaambia nyinyi pia tunasimama kinyume chenu. Sasa sijui hao viongozi wanaokuww wakristu na wanaokuwa wakatoliki wafanye nini,

waasi imani yao, wasimame upande wa serikali au watoke serikali wasimame upande wa imani yao, wachague lipi katika hayo.na kuna sababu ya kufanya uchaguzi wa ain hiyo.

Hawana nguvu za kumjibu Kardinali Pengo na wanachofanya ni kuzunguka mbuyu na kutafuta easy target!
 
Kardinali Pengo alisema hivi;
Wanazunguka mbuyu!

Umeambiwa mambo mawili
(a) Cardinal Pengo siyo msemaji wa TEC
(b) Kwa kuwa amepata amri toka juu kwenye baraza naye kwenye jimbo lake ameamuru Waraka ule wa KICHUNGAJI usomwe jinsi ulivyo.

YATOSHA MAOVU YAKE KWA SIKU - PIGA HAPANA katiba iliyoandikwa na Nyoka wa makengeza
 
aaah!!!aaaah!! ama kweli wanadhani hii ni karne ya NYEUPE ni NYEUSI..msimamo mmoja rasimu ya makengeza ina matatizo!!!
 
kardinali pengo alisema hivi;

hawana nguvu za kumjibu kardinali pengo na wanachofanya ni kuzunguka mbuyu na kutafuta easy target!

kwa taarifa yako cardinal pengo yuko chini ya rais wa tec angezuia usisomwe jimbo kuu la dsm,mbona ulisomwa huyo ni bosi wa mkombozi bank analipa fadhira,lakini sisi wakatoliki msimamo baraza la maaskofu ndio msimamo wa kanisa katoliki tanzania.
 
Umeambiwa mambo mawili
(a) Cardinal Pengo siyo msemaji wa TEC
(b) Kwa kuwa amepata amri toka juu kwenye baraza naye kwenye jimbo lake ameamuru Waraka ule wa KICHUNGAJI usomwe jinsi ulivyo.

YATOSHA MAOVU YAKE KWA SIKU - PIGA HAPANA katiba iliyoandikwa na Nyoka wa makengeza

Hakika yatosha Maovu yake kwa Siku.....Piga Kura ya HAPANA
 
Kardinali Pengo alisema hivi;

Hawana nguvu za kumjibu Kardinali Pengo na wanachofanya ni kuzunguka mbuyu na kutafuta easy target!

MwanaDiwani,

Baraza la Maaskofu ni taasisi yenye nguvu.Waraka uneshasambazwa na Pengo hana uwezo wa kuzuia
 
Last edited by a moderator:
hongera baba askofu kwa kuwakilisha sauti ya kkt
 
Kazi kweli kweli kwani haraka ya nni na haraka hiyo kwafaida ya nani?
Mbona watz mna papara hivyo? Hiyo kura yenyewe haiwezekani kupigwa hiyo tarehe 30/04/2015. Kama imechua takriban mwezi mmoja kuandisha watu ktka daftari la wapiga kura katika mkoa mmoja,

je mikoa iliobaki itachukua muda gani kwa utaratibu huu? Jiulize.! kwa hiyo kimsingi kama utaratibu wa kuandikisha wananchi kwenye daftari la wapiga kura utaendelea kufanyika kwa staili ya sasa , basi tusahau kupiga kura 30/04/2015 labda wapange tarehe nyingine!
 
Back
Top Bottom