Klabu bingwa Afrika: Esperance yatakiwa kurudisha kombe

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2018
Posts
21,711
Reaction score
35,644
Esperance wametakiwa kurejesha kombe la ligi ya klabu bingwa Afrika na kucheza mechi ya marudiano ya fainali.

Esperance ya Tunisia iliongoza kwa goli 1-0 kwenye mechi ya marudiano lakini wapinzani wao Wydad Casablanca waliondoka baada ya goli lao la kusawazisha kukataliwa

Wydad walitaka video ya wasaidizi wa waamuzi VAR kuthibitisha kama lilikua goli au la lakini mfumo wa mashine hiyo ulikua haufanyi kazi.

Shirikisho la soka Afrika (Caf) lilisema kuwa mechi ya marudiano itachezwa katika uwanja wa ugenini.

Sarri aondoka kwa 'hasira' kwenye mazoezi

Samatta: Naweza kuvaa viatu vya Lukaku Man United

Matokeo hatimaye yalisimama kuwa 1-1 kutokana na mechi ya kwanza ya Morocco

Mechi ya marudiano itafanyika baada ya michuano ya kombe la mataifa Afrika itakayofanyika nchini Misri, itakayomalizika tarehe 19 mwezi Julai.

Taarifa ya Caf imesema ''taratibu za mchezo na usalama havikufuatwa'' kwenye mechi ya marudiano na kuweka wazi kuwa wachezaji wa Esperance lazima warejeshe medali za ushindi na kombe.

Wachezaji hawakujulishwa kama mashine ya VAR ilikua haifanyi kazi
Mchezo wa marudiano uliingia dosari baada ya Waydad kufikiri kuwa wamesawazisha dakika ya 59 kupitia goli la kichwa la Walid El Karti.Goli lilikataliwa kwa madai ya kuvunja sheria za mchezo.

Mashine ya VAR ilionekana kando ya uwanja lakini wachezaji hawakuelezwa kamailikua haifanyi kazi kazi.

Hatimaye mwamuzi akatoa ushindi kwa mabingwa mara tatu, Esperance baada ya dakika 95.

Rais wa Wydad amesema timu yake ''imeathirika'' na Caf ikaitisha mkutano wa kamati kuu ambao walitoa uamuzi wa kuwepo kwa mechi ya marudiano
 
Mechi zote 2 zitarudiwa.
Ukiangalia marudio ya lile goli lililokataliwa utashangaa maana lilikuwa goli halali kabisa.
 
Mpira wa Africa hauna tofauti na siasa za Africa ni maji taka tu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…