Klabu Bingwa Afrika, Uwanja wa Taifa-Dar: Simba SC yairarua JS Saoura bila huruma goli 3-0

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001
FULL-TIME: Simba SC 3 - 0 JS Saoura

Klabu ya soka ya Tanzania Simba SC imemenyana na klabu ya JS Saoura ya Algeria katika michuano Klabu Bingwa Afrika ikiwa ni mchezo kundi D

UPDATES:

SUB ZA SIMBA: Meddie Kagere, Rashid Mtabwigwa, Deogratias Munish, Saidi Juma, Shiza Kichuya, Haruna Niyonzima

Kosi la wauaji
====

Dakika ya 37: Nahodha wa Simba John Bocco yuko nje baada ya kupata majeraha, nafasi yake ikichukuliwa na Meddie Kagere.

Dakika ya 45+3: Goooooooooooooaaaaaaaaaaal
Emmanuel Okwi anapokea pasi safi kutoka kwa Clatous Chama, anatishia anafinya kisha apiga shuti kwa mguu wa kushoto na kuiweka Simba mbele

HALF-TIME

Dakika ya 52: Goooooooooooooooooooaaaaaaaaaallll
Meddie Kagere anaiandikia Simba goli la pili akipokea pasi safi kutoka kwa Emmanuel Okwi

Dakika ya 67: Goooooooooooooooooaaaaaaaaal
Ni Meddie Kagere kwa mara nyingine tena akipokea tena pasi kutoka kwa Emmanuel Okwi. Walinzi walidhani Kagere ameotea, akatoka akanyanyua mpira kipa akishangaa tu

Dakika ya 87: Emmanuel Okwi anatoka anaingia Shiza Kichuya

FULL-TIME
 
View attachment 992342
Africa Mashariki na Kati nzima inajua,mwakilishi wao pekee atakipiga na JS Saoura katika ligi ya Mabingwa,Uwanja wa Taifa kwa Mchina.

Tutakuletea updates zote za kandanda safi la Mnyama timu tishio katika kundi D.

Usiondoke
Sema mliokuwa Dar kwa Sasa wanatuangusha Hawa tulitakiwa tuanze kuwazomea pindi wanashuka tuu uwanja wa ndege na kuonyesha tunawachinja na wakikutana na jezi za Simba tuu...Kama wao wanavyotufanyiaga tukienda kwao ila sisi tunawapokea Kama Bibi harusi vile

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu, kuwazomea toka Airport ili iweje?
Simba pia itaenda kwao ukumbuke. Wakazomewe toka Airport?
 
kwahiyo ukaona hiyo ndo njia ya ushindi??
 
kwahiyo ukaona hiyo ndo njia ya ushindi??
Ndio kazi ya shabiki hiyo maana shabiki ni mchezaji wa 12... wachezaji wanaakikisha ushindi ndani ya uwanja Mashabiki nje ya uwanja....nenda Africa kaskazini uone vitimbwi mafataki yatachomwa uwanjani tochi zitamulikwa golini kwa kipa wa timu pinzani yani vituko tupu hiyo ndio kazi ya mashabiki kama mchezaji wa 12

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani umzomee MUMEO kisa upo kijijini kwenu? We kweli hamnazo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…