Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,307
- 25,932
Klabu ya Esperance ya Tunisia(ES Tunis) jana ilifanikiwa kutetea ubingwa wa Klabu Bingwa barani Afrika baada ya kuizaba bao 1-0 klabu ya Wydad Casablanca ya Morocco kwenye mchezo wa pili na wa mwisho wa fainali uliopigwa nchini Tunisia.
Katika mechi ya awali ya fainali hiyo iliyochezwa Morocco, klabu hizo zilitoshana nguvu kwa sare ya bao 1-1. Kiujumla, Esperance wametwaa taji kwa kuwa na magoli 2-1.
Hadi lini tutakuwa wasindikizaji?
Updates:
Kamati Kuu ya Shirikisho la Soka Barani Afrika-CAF iliyoketi jijini Paris Ufaransa imeamuru kuwa mechi ya fainali ya awamu ya pili irudiwe kwenye uwanja uliopo nje ya Tunisia.
Kamati Kuu hiyo imesema mechi ya pili ilikuwa na mikanganyiko na hakukuwa na kiwango cha kuridhisha cha usalama kwenye mechi hiyo. Hivyobasi, Esperance wameagizwa kurejesha zawadi zote na kusubiri Juni 30 kurudia mtanange. Mechi ya kwanza iliyochezwa Morocco iliisha kwa sare ya 1-1.