Klabu Bingwa barani Afrika: Esperance watetea ubingwa wao

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,307
Reaction score
25,932
Klabu ya Esperance ya Tunisia(ES Tunis) jana ilifanikiwa kutetea ubingwa wa Klabu Bingwa barani Afrika baada ya kuizaba bao 1-0 klabu ya Wydad Casablanca ya Morocco kwenye mchezo wa pili na wa mwisho wa fainali uliopigwa nchini Tunisia.

Katika mechi ya awali ya fainali hiyo iliyochezwa Morocco, klabu hizo zilitoshana nguvu kwa sare ya bao 1-1. Kiujumla, Esperance wametwaa taji kwa kuwa na magoli 2-1.

Hadi lini tutakuwa wasindikizaji?

Updates:
Kamati Kuu ya Shirikisho la Soka Barani Afrika-CAF iliyoketi jijini Paris Ufaransa imeamuru kuwa mechi ya fainali ya awamu ya pili irudiwe kwenye uwanja uliopo nje ya Tunisia.

Kamati Kuu hiyo imesema mechi ya pili ilikuwa na mikanganyiko na hakukuwa na kiwango cha kuridhisha cha usalama kwenye mechi hiyo. Hivyobasi, Esperance wameagizwa kurejesha zawadi zote na kusubiri Juni 30 kurudia mtanange. Mechi ya kwanza iliyochezwa Morocco iliisha kwa sare ya 1-1.
 
Mechi ya jana imelitia aibu bara la Africa na shirikisho la soka CAF haiwezekani mechi imalizike kwa dk 61 pia inakuwaje VAR isifanye kazi mechi ya fainali .?

Pongezi kwa Wydad kwangu mimi huo ni kama ujumbe kwa madudu mengi katika soka bara Africa
 
Katetea ubingwa au kapewa ubingwa yaan refa anakataa goli alafu v.a.r inazimwa?

Sisi waafrika tupo matakoni mwa dunia
 
Caf nao wanachemka watawekaje natural ground wakati game ya kwanza ilipigwa kwa mshiriki mmoja wapo? Kama wakiweka natural ground basi matokeo ya first game yafutwe iwe mechi moja tu
 
Match inarudiwa tarehe 31 june soma vizuri
Hivi wewe unasoma comments zangu vizuri au unakurupuka tu? Nimesema najua mechi kama inarudiwa Ila caf wamechemka kuipeleka natural ground kwakuwa mechi ya kwanza haikuwa natural ground pia nayo ililalamikiwa na marefa kufungiwa, ndio nikasema ni bora mechi ya kwanza ifutwe kabisa ipigwe game moja tu
 
Ok nimekuelewa Mkuu
 
Hata ikipigwa natural ground poa tu kwa kuwa matokeo ya mwanzo ilikuwa 1-1
Kwa matokeo hayo ya mechi ya kwanza ya ugenini, Exparence walikuwa na faida ya goli la ugenini.
Inamaana ktk mechi ya pili ya nyumbani kama wangepata matokeo ya 0 0,
Inamaana wangekuwa mabingwa.
Sasa je katika kiwanja huru kukiwa na matokeo ya 0 0
Esparance watapata faida yao ya goli lao la kule ugenini ?

CAF ni lazima wabadilike, Mechi za Fainali za Ligi zao zote zifanyike ktk Neutral Ground.
Tena iwe mechi moja tu.
Wajifunze kwa wenzao wa Ulaya.
Mechi mbili ziliwekwa kimkakati wa kuzibeba timu za Waarabu.
 
Mechi ya jana imelitia aibu bara la Africa na shirikisho la soka CAF haiwezekani mechi imalizike kwa dk 61 pia inakuwaje VAR isifanye kazi mechi ya fainali .?

Pongezi kwa Wydad kwangu mimi huo ni kama ujumbe kwa madudu mengi katika soka bara Africa
Uliona mbali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…