Klabu Bingwa Ulaya: Liverpool yaiadabisha Manchester City! Barcelona mwendo mdundo

Klabu Bingwa Ulaya: Liverpool yaiadabisha Manchester City! Barcelona mwendo mdundo

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
IMG_20180405_061554.jpg


ULAYA: Klabu ya soka ya Liverpool ya Uingereza imeinyuka klabu ya Manchester City ya Uingereza goli 3-0 katika Michuano ya Klabu Bingwa Ulaya

Katika mchezo huo uliofanyia katika uwanja wa nyumbani wa Liverpool(Anfield), magoli ya Liverpool yamefungwa na M. Salah(12'), A. Chamberlain(21') na S. Mane(31')

IMG_20180405_061611.jpg


Wakati huo huo Klabu ya Barcelona ya Uhispania imeibuka na ushindi mnono wa goli 4-1 dhidi ya klabu ya AS Roma ya Italia

Barcelona ikiwa nyumbani(Camp Nou) ilipata magoli yake kupitia kwa D. De Rossi(OG 38'), K. Manolas(OG 55'), G. Pique(59') na L. Suarez(87'). Goli la Roma la kufutia machozi lilifungwa na E. Dzeko(80')

IMG_20180405_061722.jpg


Mechi hizi zote ni mzunguko wa kwanza(first leg) na watarudiana tena Aprili 10, 2018
 
Hii ni dalili UA siku za mwisho siamini city kwa ubora ule kachezea 3,,,
Na kama salah asingeumia hatari ingekua tabu
 
Liverpool FC huwa ni mabingwa wa ajabu wa UEFA Champions League, naona wameshaanza kuelekea kunako maajabu.

Vv
 
Man city na Tottenham walizoea kubebwa premier league sasa huku hamna habari hizo cheki walivoazirika ingawa bado marudiano kwa man city lakini mmhhh sijui
 
Back
Top Bottom