Klabu ya Simba SC imemtangaza kocha mfaransa Pierre Lechantre kuwa kocha wake Mkuu

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Posts
1,696
Reaction score
2,253

Klabu ya Simba imemtangaza Pierre Lechantre, kutoka Ufaransa kuwa kocha wake mkuu.

Pierre aliwahi kuiongoza Timu ya Taifa ya Cameroon kutwaa taji la Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka 2000.

======
TAARIFA KWA UMMA
Klabu ya Simba inayo furaha kubwa kuwajulisha Wanachama na washabiki wake kwamba imempata kocha wake mkuu mpya,Mfaransa Pierre Lechantre.​

Kocha huyo mzoefu ataanza kazi mara moja na atasaidiwa na kocha msaidizi wa sasa Masoud Djuma ambae alikuwa akikaimu nafasi hiyo

Kocha Lichantre keshawahi kufundisha vilabu kadhaa duniani kikiwemo kikosi cha Timu ya Taifa ya Cameroon kilichotwaa ubingwa wa Africa 2000.
Kocha huyo pia alipata kuwa kocha bora wa Afrika mwaka 2001 na pia barani Asia mwaka 2012.

Lechantre amekuja pia na kocha wa viungo Mmorocco Mohammed Aymen Hbibi, Na leo jioni kocha Lechantre ataishuhudia Simba ikicheza na Singida United kwenye Uwanja wa Taifa.

IMETOLEWA NA
HAJI S MANARA
MKUU WA HABARI SIMBA SC
SIMBA SC NGUVU MOJA
 
Klabu ya Simba Sports Club inayo furaha kubwa kuwajulisha wanachama na washabiki wake kwamba imempata kocha wake mkuu mpya, Mfaransa Pierre Lechantre.

Kocha huyo mzoefu ataanza kazi mara moja na atasaidiwa na kocha msaidizi wa sasa Djuma Masoud ambaye alikuwa akikaimu nafasi hiyo.

Kocha Lechantre wamewahi kufundisha vilabu kadhaa kikiwemo kikosi cha Timu ya Taifa ya Cameroun kilichotwaa ubingwa wa Afrika 2000. Kocha huyo pia alipata kuwa Kocha bora wa Afrika mwaka 2001 na pia barani Asia mwaka 2012.

Lechantre amekuja pia na kocha wa viungo Mmorocco Mohammed Aymen Hbibi.

Na leo jioni kocha Lechantre ataishuhudia Simba ikicheza na Singida United kwenye uwanja wa Taifa.

Imetokea na;

Haji Manara

Mkuu wa habari wa Simba SC

Simba SC nguvu moja.
 
Raia wa Ufaransa, Pierre Lechantre ameteuliwa na Klabu ya Soka ya Simba kuwa kocha mpya atakayeinoa klabu hiyo. Lechantre(67), mwaka 2016 alikuwa Kocha wa Timu ya Taifa ya Congo na mwaka 2000 aliisaidia Cameroon kutwaa kombe la Mataifa ya Afrika.

 
Duh! Upo hapa mjini tangu 2011 lakini bado hufahamu Uwanja wa Taifa upo wapi?!
 

CAF Coach of the Year
Year Manager Club/National Team
2017 Héctor Cúper Egypt
2016 Pitso Mosimane Mamelodi Sundowns
2015 Hervé Renard Ivory Coast
2014 Kheïreddine Madoui ES Sétif
..............................................
2005 Stephen Keshi Togo
2004 Okey Emordi Enyimba
2003 Kadiri Ikhana Enyimba
2002 Bruno Metsu Senegal
2001 Bruno Metsu Senegal
2000 Cecil Jones Attuquayefio Accra Hearts of Oak

CAF Awards - Wikipedia
https://en.wikipedia.org/wiki/CAF_Awards#CAF_Coach_of_the_Year
Shikamoo Manara

AFC Annual Awards - Wikipedia
 
YANGA HATUWEZI KUZIDIWA NA WANAMIKIA SIMBA ,, KAMA NI HIVYO INABIDI KUFANYIKE MAAMZI YA KUMUFUKUZA KOCHA WA SASA ILI TUMULETE ULE KOCHA ALICHUGUA UBINGWA WA AFRICA AKIWA NA IVORY COST AU TUMUCHUKUE ESCORALI WA BRAZILI..MANJI ALIPE GHARAMA ZA KOCHA LA SIVYO ANAANZA KUZIDIWA NA DEWJI

Alikuwa kocha bora wa AFCON 2000 baada ya Cameroon kutwaa Ubingwa...!
 
Alikuwa kocha bora wa AFCON 2000 baada ya Cameroon kutwaa Ubingwa...!
Dah! Kwa hiyo Manara hajui tofauti kati ya Coach of the Tournament na Coach of the Year?

Halafu kwa nini unapingana na msemaji wa klabu? Yeye si kasema KOCHA BORA WA AFRIKA 2001 na ASIA 2012? Hebu zingatia miaka, ebo!
 
Wana wivu tu ... Kocha CV inajieleza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…