Klabu ya Simba SC tupo serious tunaiihitaji saini ya Cesar Lobi Manzok, tufumbe jicho tumpe mshahara wa kuzidi milioni 40 ili aje Simba

NetMaster

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2022
Posts
1,454
Reaction score
4,925
.... 🚨 Kuhusu Cesar Manzoki iko hivi ;

Klabu ya Simba SC iko serious ikihitaji saini ya Cesar Lobi Manzoki na tayari walishafanya majadiliano kuhusu kuitumikia Simba.

Lakini klabu ya Dalian pro πŸ‡¨πŸ‡³ anayoitumikia kwa sasa imempa ofa kubwa kumshawishi Manzoki aongeze mkataba mpya. Wamempa ofa ya Tsh 40 Milioni mshahara kwa mwezi.

Wakati huohuo tayari Manzoki alishapokea ADVANCE kutoka Simba SC ili ajiunge nao dirisha hili la usajili.

Kwa hiyo uamuzi umebaki kwake, apokee ofa ya Dalian fc kisha awarejeshee pesa yao Simba au aikatae ofa ya Dalian fc kisha ajiunge na klabu ya Simba SC..

Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya klabu ya Simba, Salim Abdallah Try again amerejea kutoka Qatar πŸ‡ΆπŸ‡¦ AMBAKO alikuwa amekwenda kwa ajili ya mafunzo,, baada ya kurejea Nchini amezungumza yafuatayo katika Interview aliyofanya na Ahmed Ally.

"Watu wanaendelea kufanya makosa yaleyale, Luis Miquissone ni mchezaji wa Al Ahly πŸ‡ͺπŸ‡¬ hivyo, watu wapuuze kabisa hizo tetesi tetesi za mtaani, waachane na tetesi kutoka vyanzo ambavyo sio vya klabu yetu taarifa rasmi za usajili watazipata kutoka Simba. Usajili ni kazi ya wataalamu hivyo naomba hili tuwaachie wataalamu... Ntibazonkiza, Cesar Manzoki, Adebayor na wengine na wengine na wengine wote ambao wametajwa (Kwenye tetesi) ni Wachezaji wazuri"

"Ni kweli tutafanya usajili kwenye maeneo machache ambayo tunaona yanafaa kuongezwa nguvu.. Ila ni usajili wa nguvu Wanasimba watafurahi"

©️ Salim Abdallah 'Try again'
.

Akiwa katika ligi ya China, Manzoki amecheza michezo (11) na kufanikiwa kufunga mabao mawili (2).
 
Wachezaji wanaoimbwa sana wengi wanaishia kufulia, bora Simba waachane naye maana akija atacheza kwa pressure ili kuwaridhisha mashabiki, ikitokea mambo yakaenda tofauti kidogo atakoma kuja bongo. Simba itafute mshambuliaji mwingine.

Tumechoka mwaka mzima kila siku Manzoki upuuuzi kabisa
 
Kina chama bado wapo vizuri, hata Manzoki anaweza
 
Itabidi tutengeneze hastag kuwa Manzoki haji Simba hata kwa Dawa.

Akina Simba Naomba nopigwe ban ya Maisha JF.

Na nipo tayari kutoa hata fidia ya usumbufu


Hilo suala tumeliza Manzoki haji simba#
Wengine tukisema tunaonekana mashabiki wa Yanga. Lakini ni bora kusubiri wakati kuliko kijipa jakamoyo bila sababu. Niliwahi kuuliza; Je scouting team ya Simba striker iliyemuona na Lobi peke yake? Yaani hakuna wengine hadi tunafikiria kumlipa mshahara 50m mchezaji mmoja kwa uchumi upi? Tukumbuke mil.50 kwa mwezi ni sawa na mil 600 kwa mwaka ambayo ni bei ya wachezaji wingine 2 wa kariba yake. Kwa mshahara huo ni kwamba timu iko tayari kununua mchezaji mmoja kwa bei ya wachezaji 3?
 
Kwanza jiulize iyo pesa ya kumlipa huo mshahara wanayo, wameshaona mashabiki wao ni mbumbumbu waliotukuka kilichobaki ni wao kuwaaminisha kuwa wanamsajili manzoki ili wasahau kinachoendelea klabuni, wao watabaki kuwasajili kina ntibanzokiza wa pesa ndogo na kuvizia wachezaji wa bei rahisi lakini Manzoki awamuwezi ata kwa dawa kutokana na dau lake kuwa kubwa na mhindi wa bombay keshajiweka pembeni atoi tena pesa ya maana kwenye usajili labda klabu ikope na kudunduliza kwa wanachama ili wafanye usajili
 
Ukiona mchezaji katoka China au Uarabuni eti kaja kucheza Tz basi tambua hakuna timu inayomhitaji huko aliko pia yupo huru!! Hakuna mchezaji anaweza chomoa ofa za wachina na waarabu akaja kulipwa 10m Tz tena kwa manati, Manzoki akija Simba basi tambua hana ofa mezani.
 
Kwani sasa simba jicho mlikua mmelifungua kwa nani?

Mkifunga si ndio mtamkosa kabisa?πŸ˜‚
 
Wasije kutuletea upuuzi wa kusajili akina dejan.Mimi siwaamini tena hawa jamaa.

Si ajabu wanaleta kocha mzungu na wamemwomba aje na striker wake.
Sijui huu upuuzi wamerogwa na utopolo au nani!??

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
 
Simba ndo wamekupa taarifa kwamba hawajawaona strikers wengine hadi uwalaumu hapa?
 
Viongozi wa Simba ndo wamesema Manzoki anasajiliwa au ni viutube channels tu ndo vinakubabaisha?
Huu ni ujinga kusema kitu ambacho wahusika hawajasema wanacho wewe unasema wanacho ,
 
Hizo habari Manzoki ni propaganda, kipindi hiki ni ngumu sana kupata mchezaji wa daraja la juu (kwa kiwango cha ndani africa), labda utumie fedha nyingi sana ambazo simba hawana uwezo nazo.

Hata hivyo simba inahitaji zaidi kocha mwenye elimu,uzoefu na kipaji, atakaeweza kuwatumia wachezaji waliopo kufikia malengo ya timu, Simha inao wachezaji wenye ubora kuliko manzoki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…