Klabu ya Simba SC yamteua Method Mwanjale kuwa Nahodha mpya akichukua nafasi ya Jonas Mkude

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Benchi la ufundi la klabu ya Simba, chini ya kocha wake mkuu Joseph Omog limefanya marekebisho kwenye eneo la unahodha wa timu.

Katika marekebisho hayo yaliyoridhiwa na uongozi wa klabu, beki wa kimataifa Mzimbabwe Method Mwanjale ameteuliwa kuwa nahodha mpya wa timu ya Simba, akichukua nafasi ya Jonas Mkude atakaendelea kuwa mchezaji mwandamizi kwenye kikosi hicho, ambacho kwa sasa kipo nchini Afrika Kusini kujiandaa na msimu mpya unaotarajiwa kuanza mwezi ujao.

Kwenye mabadiliko hayo ya kawaida, benchi la ufundi pia limemteua mchezaji bora wa ligi kuu ya Tanzania na Klabu ya Simba kwa msimu huu, Mohamed Hussein (Tshabalala) na John Raphael Boko kuwa manahodha wasaidizi wa timu hiyo.

Klabu inamshukuru sana Nahodha wake kwenye msimu uliopita na mchezaji wake mwandamizi, Jonas Mkude kwa kazi nzuri alioifanya muda wote alipokuwa Nahodha wa timu.

Kwa sasa kikosi chetu kinaendelea na mazoezi na kila kitu kinakwenda vema huko kambini Eden Vale Johannesburg nchini Afrika Kusini.

*Imetolewa na
HAJI MANARA
Mkuu wa habari wa Simba
 
Duuuuuh..... Boko anakuja anakuwa Nahodha msaidizi.. Nahodha anafutwa kabisa asee ikianza migogoro ya ndani mnatafuta mchawi nani... Bado vurugu za Okwi... Asee
Soka la bongo wanaliua wabongo wenyewe. Mwandisha kasema benchi la ufundi chini ya kocha ndio limefanya marekebisho, lakini kiuhalisia ni vigogo flan ndani ya klabu ya simba ndio wanaleta shinikizo hili.
Hata hivyo sisi wacha tupige miluzi tu, maana adui siku zote muombee njaa, na ukiona jirani yako anagombana na mkewe wewe chukua jembe kalime
 
Wamemuonea tu Jonas
Hakuna uonevu hapo. Mabadiliko kwenye sector mbalimbali lazima yawepo ili kutoa changamoto za wachezaji uwanjani, kwahivyo maadam Kocha ameridhia hakuna tatizo kwavile yeye ndo anajua zaidi na hasa ukizingatia anakuwa na wachezaji muda wote!
 
Mkude alikuwa anashida gani? Duu wamemtumbua mtu aliyeipigania timu kwa moyo wake wote! Wanampa Boko unahodha msaidizi, kwa lipi waliloliona kwake! Wameshamvuruga Jonas Mkude kisaikolojia!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna uonevu hapo. Mabadiliko kwenye sector mbalimbali lazima yawepo ili kutoa changamoto za wachezaji uwanjani, kwahivyo maadam Kocha ameridhia hakuna tatizo kwavile yeye ndo anajua zaidi na hasa ukizingatia anakuwa na wachezaji muda wote!
Boko lakn kaja juzi tu
 
Manahodha wanabadilishana kama makocha, hakuna nahodha wa milele.

Mwanjali piga kazi tunajua asili yako ni Mbeya.
Mutu ya nyumbani
 
Mkude ndio amevujisha habari za Simba kufungwa goli 7,leo wamempora unahodha
 
Mkude ndio amevujisha habari za Simba kufungwa goli 7,leo wamempora unahodha
Kwahivyo Mkude ndo mwenye televisheni ilionyesha habari hiyo mpaka mkaangalia nyinyi tu Gongowazi, ambapo watu wengine hawakuona eeh..!
 
Manahodha wanabadilishana kama makocha, hakuna nahodha wa milele.

Mwanjali piga kazi tunajua asili yako ni Mbeya.
Mutu ya nyumbani
Ni jambo la kawaida sana, wakati mwingine hata akija kocha mpya hutokea kubadilisha kuanzia wasaidizi wote ambao anawakuta pamoja na Nahodha pia .. [emoji123] [emoji123]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…