Klabu ya Simba yakanusha taarifa kuwa MO Dewji ameikacha timu baada ya BMT kuzuia timu kuchukuliwa

Klabu ya Simba yakanusha taarifa kuwa MO Dewji ameikacha timu baada ya BMT kuzuia timu kuchukuliwa

RUCCI

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2011
Posts
1,701
Reaction score
1,714
Mwishoni mwa wiki iliyopita zilienea habari katika mitandao ya kijamii kuwa Mkurugenzi Mtendaji na Rais wa MeTL Group, Mohammed Dewji na Yusuph Manji wote kwa pamoja wamesitisha mipango ya kuwekeza katika klabu za Simba na Yanga.

Afisa Habari wa Simba, Haji Manara amezungumza na kipindi cha Sports Xtra cha Clouds Fm kwa upande Simba jinsi ambavyo wamelipokea jambo hilo na kusema kuwa kama klabu haina taarifa na hilo halina ukweli kwani kila kitu kinaendelea kama kilivyopangwa.

“Nimesikia hizo taarifa na kazi kubwa ya mitandao ya kijamii siku hizi ni kupotosha, hazipo official sisi kama klabu … ninavyoamini mimi hizo taarifa hazipo kwetu na sichukulii kwa uzito wowote,” alisema Manara.

Aidha amezungumza kuhusu agizo la serikali kuwazuia kufanya mabdiliko ya kimfumo ambayo yatamwezesha MO Dewji kuwekeza na kusema kuwa wao wameshapata ridhaa ya wanachama na utaratibu wa kufanya mabadiliko unaendelea.

“Serikali haikatai mabadiliko, imetoa agizo kuwa michakato hii ifate taratibu ikiwepo mabadiliko ya kikatiba ambayo klabu ya Simba imezingatia, tumeita mkutano wanachama wamesema wanataka kuingia katika mabadiliko na sisi hatuna pressure na hata MO hana pressure,

“Soon tutatoa taarifa rasmi namna mchakato huu utakavyofanikiwa kwa kuzingatia katiba ya Simba, katiba ya nchi na kanuni na sheria zinazosimamia mpira wa miguu, hatuna pressure yoyote,” alisema Manara.
 
Huyo Mo. Singida United ilimshinda atawezaje kuongoza klabu kubwa kama Simba? Aanzishe Timu yake au akanunue timu za madaraja ya chini azipandishe, kwani haoni walicho fanya Azam? Sisi kama Simba Tawi la M- Pesa hatukubaliani na huo mpango akaanzishe timu yake.
 
Mimi Nilijua Fika Kuwa Habari Zile Zilisambazwa Na Misukule Ya Chaneta FC ili kujifariji Na Mpango Wao Wa Kutaka Kuikodisha Timu Kama Masufuria...
Lakini Naona Wamecherewa Sana Coz Tunajipanga Kusherehekea Ubingwa Wa Kumaliza Ligi Bila Ya Kufungwa Gemu Hata Moja.
 
Back
Top Bottom