Klabu ya simba yapigwa faini kwa kuendekeza ushirikina licha ya kutumia mabilioni kwenye usajili

py thon

JF-Expert Member
Joined
Sep 11, 2016
Posts
2,476
Reaction score
4,448
Klabu ya Simba imepigwa faini ya sh 500k (laki 5) kutokana na timu kuingia uwanjani kwa kutumia mlango usio rasmi katika mechi ya Ligi Kuu Vodacom dhidi ya Mbao FC iliyochezwa September 21 2017.
 
Kwa kweli Klabu hii inatia aibu sana kuhusudu sana mambo ya ushirikina. Wanasema mganga wao mwaka huu kawaahidi ubingwa lakini lazima kila mechi wanayocheza lazima wavae jezi nyekundu iwe nyumbani au ugenini. Ndiyo maana kwenye mechi na Stand United walitakiwa wavae jezi zao Nyeupe lakini walizikataa na kusababisha jezi zao zifanane na zile za wenyeji.
 
Pale uwanja unitengenezwa juzi kati walifukua mauchawi gani sijui yaan eti kona zinapinda zinaingia zenyeweeee
 
Klabu ya Simba imepigwa faini ya sh 500k (laki 5) kutokana na timu kuingia uwanjani kwa kutumia mlango usio rasmi katika mechi ya Ligi Kuu Vodacom dhidi ya Mbao FC iliyochezwa September 21 2017.
Mbona yanga wanashinda kuamini uchawi daily hadi walitupa taulo la Ivo mapunda wakadai lina uchawi wala hatukuona faini hiyo. Kulikoni.
 
Hata STAND UNITED nawao wamepigwa faini ya laki5
Sababu kumuamini SANGOMA WAO[emoji3]
 
Faini ndogo mno ni kama adhabu za makosa ya ubaguzi wa rangi, faini ndogo saaaana.
 
Klabu ya Simba imepigwa faini ya sh 500k (laki 5) kutokana na timu kuingia uwanjani kwa kutumia mlango usio rasmi katika mechi ya Ligi Kuu Vodacom dhidi ya Mbao FC iliyochezwa September 21 2017.
Tukishabikia Arsenal tunaonekana sio wazalendo kumbe wapuuzi baadhi wanaleta imani za kijinga kila sehemu.
 
Pale uwanja unitengenezwa juzi kati walifukua mauchawi gani sijui yaan eti kona zinapinda zinaingia zenyeweeee
Hahaaa ile kona ya kichuya bado unaikumbuka ee? Basi uchawi unssaidia kumbe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…