Klabu ya Simba yatangaza kukamilisha usajili wa kiungo Mnigeria Victor Akpan

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Simba SC, Wekundu wa Msimbazi kutoka Jiji la Dar es salaam, leo Julai 10, 2022 wametangaza kukamilisha usajili wa kiungo wa dimba la katikati Mnigeria Victor Akpan (24) kwa mkataba wa miaka miwili akitokea klabu ya Coastal Union ya Tanga.

Kiungo huyu wa dimba la katikati (Defensore Centrale) amefanya makubwa sana akiwa na Wagosi wa Kaya kwenye Ligi Kuu msimu wa 2021/2022, akiwa amefunga na kutengeneza mabao pamoja na kuzuia.

"Kiungo wa katikati ya dimba mwenye uwezo mkubwa wa kuhimili mechi za aina zote, Victor Akpan ni Mnyama". Imeeleza kwa ufupi taarifa kutoka Simba SC.



 
sahihi haiwezekani mseme kutoka nijeria akati alikua tanga ......jamani mnashindwa kufata wachezaji Nigeria mnigeria wa tanga
Simba SC imetangaza kukamilisha usajili wa kiungo wa katikati ya dimba Mnigeria Victor Akpan (24) kwa mkataba wa miaka miwili akitokea klabu ya Coastal Union ya Tanga.

Wapi tumesema ametokea Nigeria?

Kuchangia hoja tu mnashindwa, basi hata kusoma Uzi na kuelewa nako ni tatizo..!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…