Klabu ya sokwe wakipigana ‘kickboxing’ yafichuliwa

Klabu ya sokwe wakipigana ‘kickboxing’ yafichuliwa

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
Sokwe hao wakizipiga ndani ya ulingo
KLABU moja ambapo sokwe (Orangutan) hupigana ngumi na mateke inayojulikana kama Safari World, imegunduliwa kwenye viunga vya jiji la Bangkok, Thailand.

Kampuni inayoendesha klabu hiyo iliwahi kufungiwa kufanya biashara hiyo miaka sita iliyopita.

Sokwe hao ambao huvishwa nguo za kila aina hupigana kwa nguvu huku watalii wakishangilia. Miongoni mwa sokwe hao, huvishwa viguo vya ufukweni (bikini) ambapo hufundishwa kuwa watoa huduma kando ya ulingo na wapiga kengele wakati wa mapigano hayo.

Raundi ya kwanza hiyo
Sokwe hao hupigana kikatili kwa zaidi ya dakika 30 kufurahisha watalii na baadaye hurudishwa katika matundu yao wanakohifadhiwa. Bado haijafahamika ni sokwe wangapi wamekamatwa na kupewa mafunzo na Safari World.

Waendesha kampeni ya kutetea wanyama wanasema sokwe hao ambao hufikia uzito wa kilo 113, wanaweza kufanyiana madhara makubwa wakiwa katika ulingo, na kwamba vitendo hivyo vitaharakisha kuwaangamiza kabisa katika miaka michache ijayo.

Baada ya makonde kuwa mazito, Sokwe huyu alizidiwa na kudondoka chini
Dk. Grainne McEntee, kiongozi wa chama cha kuwahifadhi sokwe cha Borneo Orangutan Survival (BOS), alishutumu kuwepo kwa vitendo kama hivyo akitaka biashara hiyo iachwe mara moja.

Mwaka 2004 serikali ya Thailand iliipiga marufuku kampuni ya Safari World kufanya maonyesho hayo baada ya kugundua ilikuwa inawatumia sokwe walioibwa kutoka Indonesia.

Huyu ndiye aliyeibuka kidedea katika mpambano huo
Baadaye sokwe 48 walichukuliwa na BOS na kupelekwa katika kituo cha Nyaru Menteng, Borneo. Kituo hicho kina sokwe wapatao 1,000 ambako inasemekana sokwe hao hufunika sura zao wanapokaribiwa na watu, jambo ambalo linaaminika kwamba watu wanaowapa mafunzo ya kupigana huwa wanawapiga pia wanyama hao.
 

Attachments

  • Orangutanskickbox1.jpg
    Orangutanskickbox1.jpg
    21.9 KB · Views: 113
  • Orangutanskickboxing2.jpg
    Orangutanskickboxing2.jpg
    32.4 KB · Views: 111
  • Orangutanskickboxing3.jpg
    Orangutanskickboxing3.jpg
    18.7 KB · Views: 100
  • Orangutanskickboxing4.jpg
    Orangutanskickboxing4.jpg
    26.6 KB · Views: 98
Back
Top Bottom