Klabu za Ligi Kuu England kuanza mazoezi yatakayojumuisha Wachezaji kugusana

Klabu za Ligi Kuu England kuanza mazoezi yatakayojumuisha Wachezaji kugusana

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,509
Reaction score
3,756
Klabu za Ligi hiyo zimepiga kura kwa siri kukubali timu kufanya mazoezi yatakayojumuisha wachezaji kugusana ikiwa ni hatua nyingine ya kukaribia kuendelea na Ligi hiyo.

Wachezaji walirejea mazoezini wiki iliyopita lakini mazoezi hayo yamekuwa yakijumuisha vikundi vidogo vya wachezaji na bila kugusana.

Mazoezi na Ligi kwa ujumla vilisimama kutokana na #CoronaVirus na sasa Uongozi wa ligi umesema wachezaji wataendelea kupimwa kila wiki mara mbili.

Hatua hii inaonesha Ligi hiyo ipo mbioni kurejea japokuwa tarehe iliyowekwa awali ya Juni 12 inaonekana itakuwa ngumu ila uwezekano mkubwa na Ligi hiyo kurejea Juni 26.

Aidha, uwezekano wa mechi za Ligi hiyo itakaporejea kuchezwa kwenye viwanja vya kila timu ni mkubwa kuliko ule wa awali kuwa mechi zitachezwa katika viwanjwa kadhaa tu.
 
Sawa

Liverpool ikifungwa huwa ninafurahi sanaa ,najisikia vibee moja hatariii

Naweza kwenda bar ku offer bia, wanywaji wote waliopo
 
Sawa

Liverpool ikifungwa huwa ninafurahi sanaa ,najisikia vibee moja hatariii

Naweza kwenda bar ku offer bia, wanywaji wote waliopo
Ila hao liverpool ata awakujui na dua lako uwa aliwafikii
 
Back
Top Bottom