Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
[TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD="align: center"]
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption"]Ukurasa wa Mbele wa Raia Tanzania
Katika uandishi wa historia ya TANU kuanzia pale kwa mara ya kwanza TANU yenyewe ilipojaribu kuandika historia yake ambayo ndiyo historia Mwalimu Nyerere na historia ya kudai uhuru, mchango wa wazalendo wengi hauonekani.
Baba yake Kleist, marehemu Abdulwahid Sykes (1924 - 1968) kwa namna yoyote ile haingii katika hao ''wengi.'' Abdul Sykes haingii katika hao wengi kwa sababu kwa ukweli khasa Abdul ndiyo ilikuwa roho ya TANU.
Chama cha TANU kiliishi na kikastawi ndani ya damu yake kuanzia alipokuwa vitani Burma wakati wa Vita Kuu ya Pili hadi aliporudi Tanganyika baada ya vita mwaka 1945 hadi alipokiasisi mwaka 1954. Katika harakati hizi za kuasisi TANU walikuwapo vijana wenzake wengi. Muhimu kuwashinda wote ni Hamza Kibwana Mwapachu (1913 - 1962) ambae alikuwa mkubwa kwa Abdul kwa miaka 11.
Ilikuwa Hamza Mwapachu ndiye aliyemfikisha Julius Kambarage Nyerere kwa Abdulwahid Sykes mwaka 1952.
Historia hii kwa miaka mingi sasa imekuwa maarufu lakini Kleist hakupata kufungua kinywa chake akaieleza kama alivyoipokea kutoka kwa baba yake.
Katika mahojiano maalum na gazeti la Raia Tanzania, Kleist pamoja na kuzungumza mambo mengi katika siasa za Tanzania, kwa mara ya kwanza kamzungumza baba yake, uhusiano wake na Nyerere na vipi Nyerere akaja kuchaguliwa kuwa rais wa TAA katika uchaguzi wa mwaka 1953 na vipi baba yake alimsaidia Nyerere hadi akafika kuiongoza Tanganyika huru.
Katika moja ya mambo ya kustaajabisha katika historia ya TANU ni jinsi Nyerere alivyoingia katika uongozi, Kwa kawaida huwa haielezwi huo uongozi ulimfikiaje na alichaguliwa katika uchaguzi upi.
Katika kuiandika historia kwa namna hii majina ya wazalendo wengi waliokuwa na Nyerere katika kuiunda TANU kuanzia mwaka 1953 pale Nyerere alipochaguliwa kuwa rais wa TAA huwa hayaonekani.
Kleist anaeleza matatizo aliyoyakabili baba yake katika kumtia Nyerere katika uongozi wa TAA na anaeleza ule ''ushindi'' wa Nyerere dhidi ya Abdul Sykes katika uchaguzi wa mwaka 1953 ulivyopatikana.
Kleist anasema ingawa baba yake alisimama dhidi ya Nyerere katika uchaguzi ule lakini katika kupiga kura baba yake hakujipigia bali kura yake alimpigia Nyerere.
Kleist anaendela kusema kuwa katika kura zilizompa Nyerere ushindi ule kulikuwa na kura tatu nazo ni ile ya baba yake, kura ya Dossa Aziz na ya Mzee John Rupia.
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]