Kluger 2900cc vs Prado 2490cc?

Kluger gari ya kishamba kuanzia design (bodi ndogo) Bei Japan (FOB) mpaka Kodi. Bila kusahau spea na Wese. Bora hiyo PRADO gari kubwa, spea za kumwaga ila nayo comfortability highway Ni mgogoro haichelew kukumwaga

Mimi ninayo lakini tangu nizaliwe sijawahi kumsikia mtu akiniambia kuwa mimi ni mshamba. Still, hata kama dunia nzima ingesimama hapa leo na kuniambia kuwa mimi ni mshamba, bado nisingechukua mtizamo wao, najijua mwenyewe nilivyo kwa mtizamo wangu mimi mwenyewe na si kwa ule wa kuambiwa na watu wengine.

Hata hivyo siamini pia kama kuna mtu mshamba kwa sababu kuamini hivyo kungenipelekea na mimi mwenyewe kuwa ni mshamba
 
Acha kujistukia. Pole lakini Kama umejisikia vibaya. Hakuna sehemu nimesema wewe MSHAMBA Bali nimesema Kluger gari ya kishamba na sababu nimeziainisha.
 
Kluger gari ya kishamba kuanzia design (bodi ndogo) Bei Japan (FOB) mpaka Kodi. Bila kusahau spea na Wese. Bora hiyo PRADO gari kubwa, spea za kumwaga ila nayo comfortability highway ni mgogoro haichelew kukumwaga
Aisee wabongo Kwa kukandia vitu vya ukweli mnatisha hivi mfano gari kama kluger inaita ya kishamba? Ebu jaribu kuendesha basi hata sikumoja alafu uje na majibu.....ingawa kila mtu ana mtazamo wake Kwenye Magari Ila Kwa gari hii kluger ni zaidi ya prado,rav 4 , vanguard na nissan X trail.

Ingawa kluger Kwenye mafuta ni jini Ila ni bonge moja la gari la kijanja
 
Ni Prado gani hiyo ya cc2490? Au zile za kizamani LC70? Maana hizi za karibuni za kuanzia mwaka 1996 engine ya chini ni cc2700.

Vile vile kuna Kluger ya cc2400 pia. So usiwaze saana. Kuhusu engine kubwa, Kluger iliuzwa US pia kama Highlander, kule kwa matumizi yao na bei za mafuta, wanapenda magari yenye engine kubwa.
 

matumizi gani ya Wamarekani yanafanya wapende magari yenye engine kubwa, kuvutana wakikwama?

au wanasanya vichwa njiani kupunguza makali ya maisha?
 
matumizi gani ya Wamarekani yanafanya wapende magari yenye engine kubwa, kuvutana wakikwama?

au wanasanya vichwa njiani kupunguza makali ya maisha?
Wanatumia saana usafiri wa barabara. Wana highways za maana zinazounganisha majimbo yao. So wanataka gari linalochanganya haraka. Ni basically same reason kama huku kwetu watu wanaosafiri sana kupendelea Land Crusiers ambazo zina engine kubwa maana zinamudu safari ndefu vizuri.
 

Landcruisers ndio zinamudu safari ndefu?

Kwani hizi Kluger, Subaru Forester, Xtrail, Mark X, Vanguard, Noah.... ukipiga nazo ndefu, Dar - Songea au Dodoma - Kigoma zinachemsha njiani?

Eeeeh?

"Wamarekani wana mabarabara mazuri kwa hiyo wanataka gari zinazochanganya haraka"!

Kwani gari kubwa ndio accelaration zinakuwa kubwa zaidi?

Hayo mambo hivi kuna mahala authoritative umesoma au ni ma fikra yako tu ya kichwani mwako???
 
Kluger bodi yake sijui imekaaje
 
Kluger bodi yake sijui imekaaje
Mkuu tema mate sababu toleo lililofuata lingekuacha mdomo wazi. Sema engine ni moja tu ya 3,500cc nafikiri hii 2AZ ilikuwa underpowered kwenye Kluger toleo la kwanza ndio maana wengi wanadai kluger ni jini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…