Hii serikali ndugu haina utu katika lolote, kama wanaweza kuua maelfu ya watu halafu wanajikausha kama hakuna kilichotokea ndio ujue hakuna wanachojali.
Kazi ya HR yeyote ni kuhakikisha demand na supply ya Human resource inabalance,Hakuna sababu yoyote ya kuzuia mtumishi kuhama kwa sababu za ajabu zinazotolewa, kwanza inasaidia kuleta brain mpya kwenye maeneo wanayohamia,Inaongeza motivation ya kazi pia
Kumshikilia mtu ambaye akili yake yote inawaza familia yake mda wate inashusha ari ya kazi hata ufanisi hauwi mzuri, ndio maana watu wanaingia kusaini wanaenda kutafuta supu akirudi saa nne ishafika anafanya kazi saa 2 anaenda lunch akirudi karibu muda wa kutoka, anajibu wateja anavyojisikia, halafu bado unahesabu una mtumishi hapo.
Ma HR wanashindwa nini kutengeneza Forum ambapo kila halmashauri au idara Inaweka wazi kada inazohitaji kuhamia,kwamba mtumishi akitaka kuhamia anajua kabisa nahitajika huko na huku anakoondoka wanajua kabisa kwamba akiondoka kuna mtumishi wa kada yake tunamkubalia anakuja kujaza nafasi.
Hapo kazi ya HR inakua kuangalia kipaumbele tu nani tumpe uhamisho kwanza mwingine asubiri kutokana na unyeti wa sababu.
Mahitaji ya kuhama hayataisha kamwe na ni haki ya mtumishi na kuzuia yana madhara sana ila sababu sio tangible hakuna anayejali, hata huu wizi na udokozi sometimes ni retaliation za watumishi tu kunyimwa haki zao anaona bora niibe tu kumkomoa mwajiri.