Uongozi wa Timu ya KMC umefika makubaliano ya kuvunja benchi la ufundi lililokuwa chini ya Kocha Mkuu, Thiery Hitimana kutokana na muenendo usioridhisha wa timu hiyo kwenye NBC Premier League.
Aidha, KMC imemtangaza Jamhuri Kihwelo Julio na benchi lake la ufundi ndio wataachukua mikoba ya kukinoa kikosi hicho.
Mpaka sasa baada ya mzunguko wa 26, KMC ipo nafasi ya 14 na alama 26 kwenye msimamo wa ligi kuu.