KMC na JKT mbona hawakutimua makocha kwanini Simba?

KMC na JKT mbona hawakutimua makocha kwanini Simba?

bryan2

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2016
Posts
3,323
Reaction score
4,679
Tangia msimu wa ligi ya NBC ligi bora kabisa Tanzania imeanza Yanga ilianza kwa style ya kipekee kabisa kwa kichapo cha dozi tano tano sijui niza Benzly penicillin(X-pen) au Benzathine Penicilin(penadur) watajua wao ila tambua hizo sindano ni mnoma zinauma sana.

Timu zilizokutana na na dozi kali kutoka kwa Yanga ni Kmc pamoja na JKt kwa hatua zile za awali kabla yanga haijastopisha dozi ya tano tano ila hizo timu zimetulia tuli wakiheshimu ubora wa Yanga hakuna timua timua kule wala kushikana uchawi.

Baada ya Yanga kupunguza dozi na kugawa dozi nyepesi za Diclofenac Injection kwa zile timu zilizokua na nidhamu na utii mkubwa kama vile Namungo, Singida Utd...nk.

Ghafla Yanga ikarudi kwenye mfumo wake wa kugawa dozi nzito raundi hii ikiwa Cetriaxone inj 5g I.m kwani mgonjwa husika baada ya kutibiwa kwa dozi ndogo bila nafuu ndipo Yanga akaenda kwenye dozi kubwa na nzito raundi hii ikimwangukia mtoto mwenye Kiburi Mjini Simba.

Yes walikua ni Simba siku ya Jumapili waliingia kwenye mtego wa Yanga na kukutana na kipondo kizito mnoo na kuungana na timu kama Zalan,Jkt, Kmc zilizokutana na hasira za Yanga.

Mbaya zaidi Simba yeye amekataa kuwa mtulivu na kuanza fukuza fukuza pale Bunju mfano mazoezi ya leo pale Bunju ukionekana unacheka tu wanajua nawe umeshiriki kuhujumu timu kwa kifupi mazoezi ya leo hakuna yeyote aliyeruhusiwa kucheka.

Je kwanini Simba wamekataa kufwata nyayo za Kmc, Jkt au Zalan kwa kutotimua makocha? mimi na wewe hatujui.

roma ikisema imesema.
 
THIMBAA NI KUBWA KULIKO keimsii na jeikeitii.
 
Hata Yanga walipopigwa.
5-0 walifukiza kocha.
4-1 walifukuza kocha
 
Back
Top Bottom