kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Kocha Moallin moja kati ya hoja zake za kuondoka kwenye timu ni kucheleweshewa malipo yake kila mwezi. Na moja kati ya majibu ya mwenyekiti wa bodi ya KMC, Meya wa Kinondoni katika kujibu hoja za Moallin ni pamoja na kusema mambo ya serikali hayana muda maalum katika kulipa stahiki mbalimbali.
Meya anataka kuhalalisha uzembe wa watendaji wa halmashauri yake uwe ni utamaduni ambao hata wageni lazima wauzoee na kuukubali. Hii haikubaliki kimataifa ingiwa Meya anataka ionekane kama ni tatizo dogo tu. Mfanyakazi anapanga mambo yake kutokana na kiasi cha pesa na lini anatazipata pesa zake. Kuchelewesha malipo iwe mshahara au bonus ni kosa kubwa katika kufanya mipango (planning). Kuchelewesha malipo ya mtumisha kunaweza pia kuchelewesha matibabu au safari ya mtumishi au mtegemezi wake, kunaweza kusababisha kukosa kiwanja, nyumba au kitu chochote ambacho kinauzwa kwa tarehe/deadline.
KMC wamekiri kuwa walikuwa wanamcheleweshea mwl na wachezaji malipo yao kwa kisingizio cha mambo ya serikali hayana uhakika wa tarehe, huu ni ujinga.