KNUT wins 50 - 60% Salary hike for Kenyan teachers!!

MTK

JF-Expert Member
Joined
Apr 19, 2012
Posts
8,924
Reaction score
6,854
Kwa wale wanajamvi wenzangu na mie wa "Shule za chini ya muuti!!"; KNUT ni kifupi cha jina "Kenya National Union of Teachers"; chama cha Walimu wa Kenya, kwa taarifa yenu leo wameshinda kesi katika mahakama ya juu kabisa nchini Kenya; The Supreme court, ambako tume ya utumishi wa Walimu nchini Kenya TSC, ilikuwa imekata rufaa kuzuia nyongeza hiyo ambayo ilitolewa na mahakama ya kazi hapo awali, TSC kwanza iliikatia rufaa kwenye mahakama ya rufaa, TSC ikabwagwa, ikasonga mbele mpaka Supreme court, Leo wamebwagwa tena na KNUT kuibuka kidedea.
Rohoni na kichwani mwangu najiuliza sana hawa Walimu wa hapa nyumbani Tanzania wana matatizo gani? Ni ubinafsi, uswahili, woga au unafiki?! Au ni " Ulofa na upumbavu" uliokithiri! Kwa miaka nenda rudi sasa tunasikia malalamiko, tishio la migomo, kufelisha wanafunzi, yote hayo wakishinikiza kulipwa stahiki zao, mazingira bora ya kazi na kupandishwa vyeo na mishahara na posho, zinaingia serikali moja mpaka inamaliza muda wake, zinaingia nyingine inatoka wao wanalalamikaga tuuu! Wakichukua hatua ni za kijikomba na kujipendekeza kwenye May day! Eti " Shemeji unatuachaje"?! Haya sasa kama na Magufuli ataingia Ikulu itabidi msubiri miaka mingine 10 mkibembeleza "Shemeji unatuachaje" kwani mkewe pia Mwalimu na yeye mwalimu!?
Nyie Walimu wa TANZANIA hii mnabembeleza kitu gani wakati ni haki yenu mnadai!? OK hata kama miongoni mwenu hakuna mtu smart na jasiri anayejua hatua mahsusi za kuchukua, hivi hata redio na TV hamsikilizagi ili mpate somo mkaombe msaada kwa jirani Kenya!! mbona Gratian Mkoba anaonekana mtu Kamanda kabisa anatosha kushughulikia shida zenu conclusively?! Walimu mmelogwa na nani au aliyewaloga kafaaa?!
Kwa Walimu wa Kenya this is not a first!, mwaka 1992 walipiga block vote kwenye uchaguzi Mkuu wa Kenya na wakasaidia sana kuifurusha serikali ya KANU na kuing'oa madarakani na kusababisha kutoweka kwa KANU kwenye ramani ya siasa za Kenya, nyie Walimu wa TANZANIA mkoje?!

Haki haiombwi, haki haitolewagi kwenye sinia la dhahabu, HAKI hupiganiwa!
Walimu wa TANZANIA acheni kusoma kijarida vya Udaku, Uhuru nazalendo, mnapumbazwa, AMKENI mpiganie haki zenu kama wenzenu wa Kenya, WORKERS OF THE WORLD UNITE AND FIGHT FOR YOUR RIGHTS, YOU HAVE NOTHING TO LOOSE BUT YOUR CHAINS?? (VLADMIR LENIN), au Walimu wa TANZANIA mmelogwa zongo hata siku za May day mnaposhikana mikono na kuimba kuhusu mshikamano huwa hamjui maana ya kitu mnachoimba mmekaririshwa tu, you are simply parroting yourselves hoarse zombies!?
Wacheni kututia aibu, piganieni haki zenu ma nyie muishi a dignified life kama watumishi mwengine, KWETU sisi tunaojua nafasi ya Mwalimu katika maendeleo ya taifa lolote, tunasononeka sana kuona jinsi taifa hili linavyowadhalilisha,rohoni tunawiwa sana kwani bila ninyi Walimu wengi wetu tusingakuwa lolote wala chochote! Chukueni hatua tutawaunga mkono.

Last but not least, Naiombea nchi yangu uchaguzi huru na haki ili Amani na utulivu vitamalaki kwani "pasipo na haki hapana Amani na utulivu Bali woga na hasira na hatimae Shari na umwagaji wa damu"
Walimu wetu Mungu awajalie ujasiri na ubunifu wa kutosha.
MTK safarini Ughaibuni kwa muda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…