Koboko (Black Mamba) - Nyoka hatari zaidi duniani

Katika uzi ambazo nimezisoma na kuzifuatilia kwa ukaribu zaidi ni huu uzi, ila kuna kitu ambacho naona wadau wote hakuna mtu alietoa tahadhari kwa kina incase ukila bite ya koboko ufanye vp kusurvive kwa huo md mfupi kabla hujafika hospitali?..
Vile vile nauliz koboko aliyekomaa anaweza kua na unene wa msitimu/ nguzo ya umeme?, na urefu wake maximum ni meter ngapi??.
Nimejaribu kufuatilia zaidi kumbe kuna nyoka mwenye sumu zaidi ya koboko anapatika hasa Australia ila mostly anaishi baharini.
 
Katika uzi ambazo nimezisoma na kuzifuatilia kwa ukaribu zaidi ni huu uzi, ila kuna kitu ambacho naona wadau wote hakuna mtu alietoa tahadhari kwa kina incase ukila bite ya koboko ufanye vp kusurvive kwa huo md mfupi kabla hujafika hospitali?..
Kwa kweli ndio maana watu wanakuwa wazito kukujibu kwa sababu huwa ni bahati kupona,ila kama utagongwa kwenye mkono inatakiwa usiunyanyue mkono wacha ukae chini ili sumu isisambae haraka,kama ukigongwa shingoni hapo hakuna jinsi ni kifo tu kama umegongwa miguuni unaweza kuwa na bahati.wataalam wanashauri usipanic kwani moyo utasukuma damu kwa haraka.
 
Nimejaribu kufuatilia zaidi kumbe kuna nyoka mwenye sumu zaidi ya koboko anapatika hasa Australia ila mostly anaishi baharini.
Mimi sikubaliani na kigezo wanachotumia kujua sumu iko kiasi gani, kigezo chenyewe ni panya wanachukua sumu halafu wana wadunga panya panya wengi watakao kufa ndio ukali wa sumu,lakini mimi nakataa, kwangu mimi Koboko ni namba Moja.
 
Nchi za wenzetu wanajua kuchangamkia fursa wakati nyoka wenyewe ni urithi wetu.
 
Sumu ya Viper tone hilo ni tosha kukuharibia uhai.
 
Huyuu balaa sumu yake ni kali 1200 times ukali wa Cyanide... Anauwezo wa kuua binadamu 26 by single bite ndani ya dak 2 tu dadekii
Hawa hata kama wana sumu kali sana ila probality ya kukutana nao ni ndogo sana kwasababu wanaisha mazingira yao
Na case zao ni chache sana kwasababu ya territory yao ni ngumu kuonana nao mara nyingi
 
Green Mamba huwa ni wadogo halafu hawana ukorofi kama Blacks haha. Kilatini anaitwa Mamba Negro.
Asante mkuu,lakini kuhusu sumu vipi
nao sumu yao ni kali au wao ni poa
kama muonekano wao ulivyo?
 
Hawa hata kama wana sumu kali sana ila probality ya kukutana nao ni ndogo sana kwasababu wanaisha mazingira yao
Na case zao ni chache sana kwasababu ya territory yao ni ngumu kuonana nao mara nyingi
Kila jumapili na ijumaa watu wanapoenda beach ni kama unaenda kuonana nao labda kama hujui kuogelea.
 
Asante mkuu,lakini kuhusu sumu vipi
nao sumu yao ni kali au wao ni poa
kama muonekano wao ulivyo?
Sumu zao ni kama sawa tu ila Green Mamba ni mpole sana na unaweza kulala nae chumba kimoja bila ya shida yoyote.
 
Mimi sikubaliani na kigezo wanachotumia kujua sumu iko kiasi gani, kigezo chenyewe ni panya wanachukua sumu halafu wana wadunga panya panya wengi watakao kufa ndio ukali wa sumu,lakini mimi nakataa, kwangu mimi Koboko ni namba Moja.
Sasa mzee wa kazi wanasema no research no right to speak!. Wenzetu wako advanced sana hata kama wanatumia panya kufanya research mwisho wa siku wanakuja na observation na ndo mana wamepanga top ten ya most venom snake ,inamanisha waliona matokea yke baada ya kuwadunga mmoja baada ya mwingine.
 
Nyoka husikia kivyao sio viziwi kabisa kama baadhi ya watu wanavyoamini,kuna baadhi ya nyoka wanaona mpaka kwenye giza,kitu ambacho binaadamu wamegundua juzijuzi,halafu nyoka anatumia ulimi wake kulamba harufu vizuri kuliko pua zetu.
Hapo sasa kwenye ulimi ndo utajua maajabu ya Mungu.
Anapotoa ulimi nje na kuuingiza ndani
ana kisehemu kinaitwa "Jacob son" anapogusisha ulimi
wake anapata taarifa za kitu kilichopo mbele yake
kama kina madhara au la.Ndo maana tunashauriwa
unapokuta na nyoka usiwe na mawazo ya kutaka kumdhuru,
Tulia tuli utaona anaanza kuondoka kama hajachokozwa
kabla ya kukutana na wewe.
 
Kuna wataalam wengine kutoka Afrika ya kusini pia wanakataa na mimi nawaunga mkono.
 
Ngoja utafiti mpya uje uone kuwa Koboko anapewa nafasi yake adhim.
 
Kuna sehemu nimesoma Koboko ndio aliwaua sana Wajerumani enzi za mashamba ya mikonge mpaka wakawa wanafikiri ni nyoka wa mizimu ya kiafrika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…