Koboko (Black Mamba) - Nyoka hatari zaidi duniani

Wanaokaa kwenye miti kumendea utosi si ni green mamba hao
Hata hawa wanapenda sana kukaa kwenye miti ipo sehemu nilisoma kwamba akiwa ameshiba hupenda sana kukaa juu ya miti.shimoni na kwenye mapango huingia kutafuta chakula tu.

Pia kutokana na urefu wake na mwili strong huweza kuhama mti mmoja kwenda mwengine bila shida so anaweza nusu ya mizunguko yake kwa siku kama ameshiba akauitumia juu ya mti so ukijichanganya ukakatiza alipo anakutusua.
 
Huo ni uwongo sijui umezitoa wapi hizo data zako.Black mamba huwa hawazidi mita 3(Futi kumi) sasa wewe hizo futile 16 umezitoa wapi.Ni kweli ni nyoka mwenye spidi kuliko wote na ila sio kweli kwamba kuna maeneo anachagua ya kung'ata ni kweli nyoka mrefu anaweza kung'ata sehemu ya mwili anayeweza kuifikia ila sio kwamba anachagua sehemu maalumu za kung'ata.Hakuna nyoka ambaye akikung'ata unakufa ndani ya dakika hizo ulipolitaja kwa maana sumu inachukua muda kuzunguka kwenye mfumo wa damu.

Wataalamu wanasema huyu nyoka sumu yake inachukua dakika angalau 20 kukufanya uwe mfu.Nyoka huwa sio rahisi akufuate ulipo akugonge mara nyingi akikuona huwa anikimbi ila ukimsogelea nae anaanza kujihami na kama yuko kwenye mti unapita chini anaweza kufoka au kukaa kimya.

Hizo Hadithi za kutembea na chungu chenye hot liquid ni nonsense.Ni kweli pia kwamba anaweza kung'ata zaidi ya watu kumi kwa mara moja.Unaweza kujiuliza kwanini anaitwa black mamba wakati sio mweusi.Anaitwa black mamba kwasababu kule ndani ya mdomo ni kweusi na anapofoka akiwa ameachama utaona kuna weusi ndani ya mdomo
 
Somo zuri Tunashukuru.
 
Maelezo yako yapo sahihi mkuu ila black mamba ni tofauti kidogo kuhusu suala la kushambulia. Kawaida nyoka hua hashambulii bali hukimbia amuonapo binadamu. Black mambi na tofauti kidog kwani yeye ukiingia kwenye territory yake( ni territorial snake) anakufuata na asipokuelewa anakushambulia kwa kukugonga tena wakati mwingine several times
 
Kofia ngumu je akikupapasa shingoni ushahisi kitakachokutokea mkuu?maana bora chungu akishuka akikigusa hata kwa bahati mbaya atakuta nacho ni cha moto atainuka juu hiyo kofia ngumu akiigusa si ndo atatelezea hapo shingoni.

Duuh noma tupu, ukichimama nchale ukichutama nchale.... ni bora kujiepusha tu na maeneo yao.

Nafikiria ikiwa mtu inabidi aandae chungu ni kwamba anajua kabisa hao jamaa wapo, sasa hicho chungu kichwani kinatulia bila kushikilia mikono.?

Aaah, hapana..!!
 
Ila hata wewe bado hujui baadhi ya tabia za nyoka wakubwa, kama, chatu, Swila, black mamba, (Koboko). Green mamba, Cobra.

Hawa ni jamii ya nyoka ukimkuta aliye mkongwe hasa, huwa hangojei umsogelee, anauwezo wa kukufuatilia hata ukiwa umbali wa mita 70, ilimradi ahisi tu huko kuna mwanadamu.

Mimi binafsi nimesha kimbizwa sana hasa na Swila huko maporini, enzi hizo za ujana wangu.

Mara nyingi nyoka wakubwa wana tabia ya kuishi eneo moja, kama anaishi karibu na barabara au njia, mara nyingi wapitaji humuona nyakati maalumu, wakati wa jua la asbuhi hupta jua, na jua la machweo.
 
Kama mlikuwa hamjui pia ni kwamba huyu jamaa ni mtafunaji mzuri sana wa bangi na ndio maana akili yake wakati mwingine sio nzima, akikuona tu yeye anawaza ambush, yaani akuvamie akugonge tena sio mara moja yaani kama ni ngumi tunasema anakupiga mikito hata kumi kwa mkupuo.
 
Nyoka huwa anafuata harufu kwa kukusanya chembechembe za harufu zilizopo kwenye hewa kwa kutumia ulimi akishautoa ulimi nje akiurudisha ndani unagusa kwenye Jacob's organ hapo ndipo anaifuata harufu na sio kwamba anakufuata binadamu eti akutie meno acheni kudanganyana,nyoka anatafuta mawindo kwa njia ya harufu. Halafu kingine unachodanganya huyo nyoka ana speed kuliko wewe angekuwa umefukuzwa mara nyingi hivyo kama unavyodai naamini siku moja ungekuwa umekula jino hata la kalio.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…