Koboko (Black Mamba) - Nyoka hatari zaidi duniani

huyo mtaalam... huwa hafanyi makosa akiwa kazini, kipind cha zaman kidogo.... wazungu walienda tabora... wakasikia habari ya kiumbe huyu( kama ilivyo marufuku kumtaja jina)... wakabisha sana juu ya habar zake... maana wao walikuwa wanaamin hakuna kama cobra..

shauku ilivyowajaa... wakatoa dau zuuri... kwa kijana atakayemkamata 'mtaalam' na kuwaletea..... ghafla akajitokeza masai mmoja kwa kujiamin.. kuwa wampe siku tatu... atakuwa ameshamkamata....

masai akazama vichakani.... katika kupitapita... akamkuta mtaalam anakula asali..... masai akamvalisha gunia mtaalam pamoja na mzinga wa asalii.....

aisee... itaendelea... nisije nikafungua uzi ndan ya uzi....
 
Huyu ni black mamba kwa jina lingine ni mweusi wa kung'aa na jina hili la black ni kwa sababu ndani ya mdomo wake ni mweusi sana na cha ajabu akipanua mdomo utafikiri jeneza.
Hapana mkuu umechanganya kidogo, huyu koboko ni puff adder kama sijakosea huwa ni mfupi na mnene. Black mamba ni mrefu na mwembamba ndie huwa anaitwa kiss of death
 
Koboko ana hasira sana ukikutana nae ni kutambika kikwenu au sala ya mwisho.
Usithubutu kukimbia kwani ana mbio za ajabu na kama kuna matuta ukajifanya kuyaruka yeye anatambaa juu ya matuta umenielewa
Ukiwa na gari ukamuona barabarani ataifukukuza gari na kuingia kwa chini na kujificha mpaka kwako
Hasira za kurushwa akitoka hapo ana uwezo wa kuuwa watu 25 kwa mkupuo na sumu yake huvuki dakika 30 ulimi nje.

Nawapenda nyoka lakini huyu sio rafiki kabisa very aggressive
 
Hapana mkuu umechanganya kidogo, huyu koboko ni puff adder kama sijakosea huwa ni mfupi na mnene. Black mamba ni mrefu na mwembamba ndie huwa anaitwa kiss of death
Puff adder ni kifutu ambae ni mfupi na wanauwa sana kuliko hata koboko
Koboko ndio huyu wanaogopa hata kumtaja jina na ndio huyu black mambas
Huyu hapa anaezungumziwa
Hebu msome kidogo
 
Mambas ni aina ya nyoka wenye sumu kali na wenye hasira na kasi japokuwa wapo nyoka wengine wenye sumu kali zaidi, lkn katika ukanda wa tropik ni jamii hii ya nyoka ndiyo wabaya zaidi, huweza kushambulia hata kundi la mifugo.
 
Hizo ni figure of speech tu !una asilimia 99 ya kushinda vita dhidi ya nyoka wakati una less than 10% au no chance at all kushinda vita dhidi ya simba na chui
 
Puff adder ni kifutu ambae ni mfupi na wanauwa sana kuliko hata koboko
Koboko ndio huyu wanaogopa hata kumtaja jina na ndio huyu black mambas
Huyu hapa anaezungumziwa
Hebu msome kidogo View attachment 766058
Hivi koboko kwanini watu hawamtajitaji hovyo ni kwa namna alivyo na sumu kali, na kwa hapa Tanzania wapo maeneo gani hasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…