Koboko (Black Mamba) - Nyoka hatari zaidi duniani

Unajua kilichowashangaza watu ni kuwa huyu nyoka ni wakufugwa na huwa wanajua saa ngapi ana njaa ndio wanamuwekea msosi kwa mshangao wao badala ya kumla akamfanya rafiki ilibidi baadae wautoe msosi huo wakauleta mwingine ukaliwa.
 
Taya la chini la nyoka sio solid kama letu linaachana katikati ili mlo uweze kuingia.
 
Reactions: Cyb
Ukifanikiwa kumuua Koboko kata kichwa kwanza,Daudi pichani alimzika koboko mdogo akifikiri keshamuua Koboko akakurupuka Daudi akakimbia.
 
Koboko aliyekomaa huwa anagonga kuanzia mabegani na kichwani,hayo maeneo ni venom inasafiri haraka kwenda kwenye moyo.
Halafu unakuta kuna watu wana amini kuwa koboko anagonga kichwa tu na sio kwingine.
Ndio maana ukawasikia wanasema tembea na chungu cha uji wa moto
Sasa kwa siku hizi naona wangejiongeza tu wavae helmets kila saa
 
Halafu unakuta kuna watu wana amini kuwa koboko anagonga kichwa tu na sio kwingine.
Koboko akiwa mrefu aliekomaa akisimama katika mashambulizi anafikia kichwani shingoni kwa urahisi sana,na ukisha anguka anaanza kugonga pipote kwenye mwili.
 

Koboko kama huyu alivyokomaa anauwezo wa kukugonga kichwani ndani ya sekunde mbili,na kama kuna miti karibu huwa anatembea huu ya miti huku akipambana.
 

Hili eneo lina Koboko mkubwa aliyekomaa na huwa anawagonga wanyama mbalimbali na kuwauwa huyu Pongo ni mmojawapo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…