KOCHA AL-MERREIKH: Yanga inacheza kama vilabu vikubwa Ulaya, Watabeba Ubingwa

Smart codetz

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2023
Posts
218
Reaction score
875
Kocha wa klabu ya Al Merreikh, Osama Nabih amesema Yanga SC inacheza kama vilabu vikubwa vya Ulaya na kubainisha kuwa hatashangaa ikiwa Yanga itatwaa ubingwa wa Afrika.

“Tumekutana na vilabu vikubwa vya Afrika, lakini tulivyocheza dhidi ya Yanga, tumeona ubora wao wa kipekee.

“Sitashangaa ikiwa Yanga itatwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu. Wanacheza kama vilabu vikubwa vya Ulaya." amesema Osama Nabih.

Al Merreikh imeondoshwa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kufuatia kipigo cha jumla cha 3-0 dhidi ya Yanga kwenye hatua ya pili ya mtoano.

20231001_171206.jpg
 
Yanga mko vizuri sema na bahati inachangia mnakutakana na Timu ambazo haziko stable kwa wakati huu ,unacheza na timu Chamazi halafu unaita ugenini au kigali timu ya Sudani .

Ila kiujumla Mna kikosi kizuri na kocha mzuri ,Simba wachezaji wapo ila kocha hakuna .
 
Tuwekee clip mkuu tusikilize hapo. Hapo ni sawa na kuweka picha then uulize picha hii inamaanisha nini?
 
Kocha wa klabu ya Al Merreikh, Osama Nabih amesema Yanga SC inacheza kama vilabu vikubwa vya Ulaya na kubainisha kuwa hatashangaa ikiwa Yanga itatwaa ubingwa wa Afrika.

“Tumekutana na vilabu vikubwa vya Afrika, lakini tulivyocheza dhidi ya Yanga, tumeona ubora wao wa kipekee.

“Sitashangaa ikiwa Yanga itatwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu. Wanacheza kama vilabu vikubwa vya Ulaya." amesema Osama Nabih.

Al Merreikh imeondoshwa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kufuatia kipigo cha jumla cha 3-0 dhidi ya Yanga kwenye hatua ya pili ya mtoano.

View attachment 2768634
Ulaya ya Kilosa Morogoro ama Ulaya hii ya Europe.
 
Yanga mko vizuri sema na bahati inachangia mnakutakana na Timu ambazo haziko stable kwa wakati huu ,unacheza na timu Chamazi halafu unaita ugenini au kigali timu ya Sudani .

Ila kiujumla Mna kikosi kizuri na kocha mzuri ,Simba wachezaji wapo ila kocha hakuna .
Raja alicheza na nyie Rwanda?
 
Inacheza vizuri - Ndio
Inacheza kama timu za Ulaya - Mmmmh, labda kama Man U
Itachukua ubingwa wa Afrika - Hebu kocha turudishie viingilio vyetu
 
Mnaobisha Fuatilieni, Jamaa kweli kaongea, tena kwa kumaanisha...

Hio Clip ipo mpaka kwenye Website ya Man U.
 
Kocha wa klabu ya Al Merreikh, Osama Nabih amesema Yanga SC inacheza kama vilabu vikubwa vya Ulaya na kubainisha kuwa hatashangaa ikiwa Yanga itatwaa ubingwa wa Afrika. “Tumekutana na vilabu vikubwa vya Afrika, lakini tulivyocheza dhidi ya Yanga, tumeona ubora wao wa kipekee.
El Merrikh kila wakiingia makundi wanakuwa wa mwisho
 
Back
Top Bottom