Kocha Amunike aanza kujuta kuwatimua nyota wa Simba

Kocha Amunike aanza kujuta kuwatimua nyota wa Simba

Lupweko

JF-Expert Member
Joined
Mar 26, 2009
Posts
23,566
Reaction score
24,891
Kocha wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Emmanuel Amunike, amesema kumkosa mlinzi wa pembeni, Shomari Kapombe katika kikosi chake ni pigo kubwa
Akizungumza baada ya mazoezi ya juzi jioni yaliyofanyika Uwanja wa Boko, Amunike alisema pengo la Kapombe ni kubwa lakini atajitahidi kuangalia mchezaji wa kuliziba
Alisema Kapombe ni beki mwenye uwezo mkubwa, alifuatilia mechi alizocheza Ligi Kuu ya Tanzania Bara na kuona kiwango chake, alitamani kuwa naye katika kikosi hicho lakini hana uwezo wa kumrudisha
“Kapombe ni mchezaji mwenye uwezo mkubwa, anaamua nini amfanye adui anapokuwa uwanjani, kiukweli hazungumziki lakini ni mtu ambaye ameniachia pengo”, alisema kocha huyo raia wa Nigeria

Source:

kpm.png
 
Anatafuta sababu tu,, tunataka ushindi sio visingizio,,
 
Kashaanza kutafuta sababu huyo. Si alijifanya yeye ni mwalimu wa nidhamu badala kuangalia ushindi. Apambane na hali yake. Okwi akiifunga Starz mimi nitatamani kulia ila machozi hayatanitoka.
 
Simba imeweka mkakati wa pamoja wakugomea timu ya taifa kimtindo ili wapumzike wajiandae na ligi.....wanakwepa kupata fatique
 
hayo ni matokeo ya maamuzi ya kukurupuka
 
Back
Top Bottom