Kocha Amunike awaondoa wachezaji wa Simba Taifa Stars kwa kuchelewa kuripoti kambini

Kocha Amunike awaondoa wachezaji wa Simba Taifa Stars kwa kuchelewa kuripoti kambini

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Wachezaji wa Simba SC ambao Waliitwa kwenye timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars, wameondolewa kwenye kikosi hicho kwa kushindwa kuripoti kambini kwa muda uliotakiwa

Wachezaji hao ni Shomari Kapombe, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, Hassan Dilunga, John Bocco na Shiza Kichuya ambao wote walitakiwa kuripoti kambini jana usiku lakini Aishi Manula pekee ndiye aliyeripoti

Kocha Emmanuel Amunike ametoa msimamo huo, kwamba hataki wachezaji wasiojitolea kwa ajili ya timu yao Taifa.

Wachezaji walioitwa kuchukua nafasi ya wachezaji wa Simba kwenye kikosi cha Taifa Stars ni Salum Kimenya, Paul Ngelema, David Mwantika, Salum Kihimbwa, Ali Abdulkadir, Kelvin Sabato, Frank Domayo.

Mbali na wachezaji hao viongozi wa Simba, Hamisi Kisiwa na Meneja Richard Robert watapelekwa katika Kamati ya Maadili ya TFF siku ya Jumamosi ili kuchukuliwa hatua

Timu ya taifa (Taifa stars) inaingia kambini kujiandaa kupepetana dhidi ya timu ya taifa ya Uganda katika kufuzu michuano ya AFCON.

IMG_20180829_130948_159.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kama kosa ni la klabu kushindwa kuwaruhusu mapema klabu ipewe adhabu kali
 
Wachezaji wa Simba SC ambao Waliitwa kwenye timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars, wameondolewa kwenye kikosi hicho kwa kushindwa kuripoti kambini kwa muda uliotakiwa

Mchezaji pekee wa Simba ambaye ameripoti kambini ni Aishi Manula huku wengine wakiwa hawajatoa sababu.

Kocha Emmanuel Amunike ametoa msimamo huo, kwamba hataki wachezaji wasiojitolea kwa ajili ya timu yao Taifa.

Wachezaji walioitwa kuchukua nafasi ya wachezaji wa Simba kwenye kikosi cha Taifa Stars ni Salum Kimenya, Paul Ngelema, David Mwantika, Salum Kihimbwa, Ali Abdulkadir, Kelvin Sabato, Frank Domayo.View attachment 850297

Sent using Jamii Forums mobile app
Dalili za mvua ni Mawingu...huyo kocha kashindwa day one tayari...yeye alivyokuwa timu ya taifa ya Nigeria akichezea vitimu vya "chokochokoroni" wakati akiwahi kambini huku wakina Finidi Geogre na Kanu wakichelewa kambini kutokea Ulaya..walifkuzwa? huyu hatufai tayari
 
Dalili za mvua ni Mawingu...huyo kocha kashindwa day one tayari...yeye alivyokuwa timu ya taifa ya Nigeria akichezea vitimu vya "chokochokoroni" wakati akiwahi kambini huku wakina Findi Geogre na Kanu wakichelewa kambini walifkuzwa? huyu hatufai tayari
Huyu atachemka tu. Mbona akina Samatta bado hawajaripoti, hazijui fitina la soka la bongo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dalili za mvua ni Mawingu...huyo kocha kashindwa day one tayari...yeye alivyokuwa timu ya taifa ya Nigeria akichezea vitimu vya "chokochokoroni" wakati akiwahi kambini huku wakina Finidi Geogre na Kanu wakichelewa kambini kutokea Ulaya..walifkuzwa? huyu hatufai tayari
Pumba hizi zote ni zako?

acha hizo ushindi ni pamoja na nidhamu na sio kuijiona bila wewe timu haifiki kokote
 
acha hizo ushindi ni pamoja na nidhamu na sio kuijiona bika wewe timu haifiki kokote
Pomoja na hivyo mkuu, kumbuka akina Chilunda, Samatta, Mao, Msuva, Banda..Hawajaripoti na wachezaji wa Simba sio kwamba wamegoma wamechelewa tena masaa.

Tuangalie na upande wa pili, hiyo imo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kocha anatuchokoza huyu sasa subiri tutaendelea kuzomea taifa stars
Timu ya taifa wachezaji wakiitwa lazima wapewe na posho za kuwafikisha kambini hilo halijazingatiwa kocha anakurupuka tu
Day one failure
 
Naona Kaingia na LUGOLA STYLE
Ukichelewa unatimuliwa. Je kesho hao hao waliobaki wakitangaza kujiuzulu atacheza yeye,
Lkn pia akumbuke kitendo cha kuengua wachezaji wa klabu mojawapo kubwa tayari ametengeneza Upinzani kwa mashabiki wa Upande huo hawatamuunga mkono kivile kama sio kuzomea. Litazamwe upya hili.
 
Back
Top Bottom