Kocha Denis Lavagne Atupiwa Virago Azam FC

Kocha Denis Lavagne Atupiwa Virago Azam FC

Shark

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2010
Posts
29,775
Reaction score
29,746
FB_IMG_16664949022910410.jpg

T A A R I F A

Bodi ya Azam FC imesitisha mkataba na Denis Lavagne, kama kocha mkuu, kuanzia leo, Oktoba 22, 2022.

Uamuzi huo ni kwa maslahi mapana ya klabu na mustakabali wa mradi wake wa maendeleo ya kiufundi.

Denis Jean Lavagne, raia wa Ufaransa, alijiunga na Azam FC Septemba 7 mwaka huu akisaini mkataba wa mwaka mmoja uliomtaka aifikishe klabu kwenye angalau hatua ya makundi ya mashindano ya Afrika.

Kwa bahati mbaya mahitaji hayo ya kimkataba hayakufikiwa hivyo bodi ikafikia uamuzi huu.

Kwa sasa timu itakuwa chini Kalimangonga Sam Daniel Ongala na Agrey Moris hadi hapo itakapotangazwa vinginevyo.

Bodi inamshukuru Lavagne kwa jitihada zake za kuisaidia klabu yetu na weledi mkubwa aliouonesha alipokuwa nasi.

Aidha inamtakia kila la heri huko aendako.

#WeAreAzamFC
#TimuBoraBidhaaBora
 
Azam mngesuburi hadi baada ya mechi yenu dhidi ya Mnyama Mkali Mwituni, Simba SC hapo 27/10 ndo mmtimue Kocha.

Kwanini nasema hivyo? Tarehe 27/10 tutawapiga kama ngoma, na kitakachotokea mtawatimua hao wakina Ongala na Morris. Sasa hamuoni hamtakua na hata na kocha wa muda? Anyway mda utaongea.
 
Kwa timu gani uliyo nayo, mkicheza leo mna pigwa kama ngoma azam pia atapiga kwenye mshono.
 
Tatizo la Azam sio kocha,hata mkimleta Guardiola mwembamba haitasaidia kitu
Wachezaji wa Azam ni sawa na watoto vilaza wa Tajiri ambao baba yao sababu ya uwezo wake anajitahidi kuwatafutia shule nzuri na walimu wazuri lakini watoto bado mbumbumbu
 
Wachezaji wa Azam ni sawa na watoto vilaza wa Tajiri ambao baba yao sababu ya uwezo wake anajitahidi kuwatafutia shule nzuri na walimu wazuri lakini watoto bado mbumbumbu
Shida sio watoto,shida ni wazazi,pamoja na utajiri mzazi hajui kulea
 
Azam inasikitisha sana. Bora Mzee Bakhresa arudi Simba washirikiane na Mo au Mo ampishe Bakhresa.
 
Azam walicheza vizuri mechi na Yanga tu. Baada ya hapo, wakaanza kuruka ruka tu uwanjani.
 
Azam haihongi marefa ndo tatizo lilipo
 
Simba msijidanganye mtafunga Yanga kirahisi ivyo,mna kikosi cha kawaida sana,battle itakayo tokea leo pale hutaamini.
Kwani tumesema wapi tutamfunga kirahisi

Inaonesha unaamini UTO atafungwa ila sio kirahisi

Asante sana kwa kuliona hilo.
 
Back
Top Bottom