Kocha Amunike ametoka kwao kuja kutuharibia Taifa Stars. Kawaacha Afcon Ajibu na Mouse eti hawana nidhamu. Tumeona makocha wangapi wakifanya kazi na wachezaji wasiokuwa na nidhamu lakini wanacheza vizuri. Mchukue Mario Balloteli. Yeye ni kichaa kabisa lakini makocha Wa Italia hawamwachi. Pia waangalie Romario wa Brazil, Gatuso wa Italia na Diego Simone kocha wa Atletico Madrid. Wote enzi zao walikuwa watata lakini walichezea timu zao za taifa hadi walipozeeka. Kuwa kochi ni pamoja na kuhimili wachezaji watukutu. Amunike hana lolote anapenda kuabudiwa