19792magufuli
New Member
- Feb 21, 2023
- 1
- 5
Kocha huyu ingawa kwangu ananipa mashaka sana kutokana na sub zake lakini haiondoi ukweli kuwa amevunja rekodi ambazo hazijawahi kuwekwa na kocha yeyote aliyewahi kufundisha Simba.
Fahdu ameweka rekodi kubwa tatu ambazo mtu yeyote wa mpira anipinge kwa takwimu na sio porojo.
1. Fact ya kwanza kwa kocha huyu ni kupata goli katika mechi zote za ugenini, kumbuka Simba ilikuwa inashinda sana home na ikienda ugenini kupata goli ni mtihani, huyu mtu kusema kweli amejitahidi maana mechi zote za ugenini Simba imepata bao.Kule kwa Constantine Tshabalala alifunga, kule Tunisia Jeans Charles Ahoua akaweka kambani na jana kule Angola Leonel Ateba Mbida.
2.Rekodi ya pili kwa kocha huyu ambayo haijawahi kufikiwa na kocha yoyote aliyewahi kufundisha Simba ni kufuzu hatua ya robo fainali ugenini tena tukiwa na mchezo mmoja mbele.Kwa kweli makocha wengi waliowahi kufundisha Simba hili liliwashinda, tulikuwa tunaenda kucheza lakini mwishoni fainali ni uwanja wa Mkapa, tukaanzisha Kwa Mkapa hatoki mtu, Do or Die.
3. Rekodi ya tatu kwa kocha huyu ni kwa Simba kucheza soka inayoeleweka.Kiukweli japokuwa tuna shida sehemu ndogo ndogo sana lakini ukweli kuwa kiwango cha timu yetu ni kizuri sana, mpira unaanzia kwa Pin Pin Camara, anamrushia Kapombe anarudisha kwa Camara, anapeleka kwa Kagoma anaivusha kwa Mpanzu, anamlamba chenga mzembe mmoja wa Bravos anaivusha kwa Kibu, inaletwa kwa Mavambo inapelekwa kwa Kapombe anaitupia kwa Ateba anauweka wavuni.
Rekodi hizo ni unprecedented kwa kweli.