Kocha Julio: Wametupa mchezaji kwa mkopo halafu wameweka masharti tukikutana asicheze, huu ni ushamba

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Kocha Msaidizi wa Namungo FC, Jamhuri Kihwelo Julio, amelalamikia kipengere cha mchezaji wa mkopo kutocheza wakati timu hizo zinapokutana.

"Mpira wa Afrika una mambo mengi ya kishamba utakuta timu inakupa mchezaji kwa mkopo halafu inakupa masharti tukikutana tusimtumie mchezaji huyo, nini hiyo sasa kama si uoga na ushamba.

Azam FC wametufanyia kitu cha kishamba, wametupa mchezaji Emmanuel Charles kwa mkopo lakini wameweka kipengere tukikutana na Namungo FC asicheze, mambo haya hata Ulaya hayapo".

Julio aliyasema hayo baada mchezo wa NBC kati ya Namungo FC na Azam FC ambapo Namungo FC walipoteza kwenye dimba lake la nyumbani kwa mabao mawili kwa moja.
 
Hii ni sheria Ni kwa ajili ya kukwepa hujuma na upangaj wa matokeo.

Club nyingi duniani,
Mchezaji akichukuliwa kwa mkopo, mshahara wake anaendelea kulipwa na kule mlikomkopa.

Sasa mkimpanga kwny mechi akawahujumu kwa kufeva boss wake mtalaumu Nini pale?
 
Mikataba yamkopo hua na vipengele vyake hata huko ulaya Kuna wengne vinaruhusu kukutana na parent club na wengne wanakataza so huo Ni maamuzi yenu timu zote mbili na vile vile maswala yamshahara nimakubaliano pia wengne hulipa yote wengne hulipwa na klabu ya awali wengne wanachangia so hizi zote Ni agreement tu
 
Hivi anazungumzia Ulaya ipi? Conor Gallagher wa Chelsea yupo Crystal Palace wala hachezi game dhidi ya Chelsea kwasababu ya hicho kipengere.
 
Mbon nae anaropoka tu huo si mkataba na namungo alikubari kingine unaweza kukuta uyo mchezaji bdo anaripwa n azam
 
Mikataba yamkopo hua na vipengele vyake hata huko ulaya Kuna wengne vinaruhusu kukutana na parent club na wengne wanakataza so huo Ni maamuzi yenu timu zote mbili na vile vile maswala yamshahara nimakubaliano pia wengne hulipa yote wengne hulipwa na klabu ya awali wengne wanachangia so hizi zote Ni agreement tu
Hivi hicho kipengere amekiona wakati anataka kumchezesha au kabla?
 
Hii ni sheria Ni kwa ajili ya kukwepa hujuma na upangaj wa matokeo.

Club nyingi duniani,
Mchezaji akichukuliwa kwa mkopo, mshahara wake anaendelea kulipwa na kule mlikomkopa.

Sasa mkimpanga kwny mechi akawahujumu kwa kufeva boss wake mtalaumu Nini pale?
Sasa we mtu mwenyewe julio anaelewa unadhani yeye anapenda sana maiki na camera
 
So tuseme julio kajipakata kutokujua mambo ya dunia amejikuta kaongea ugoro
 
Back
Top Bottom