Kocha Julio: Wametupa mchezaji kwa mkopo halafu wameweka masharti tukikutana asicheze, huu ni ushamba

ipo hata kwenye EPL.... wanaaita BEING CUP TIED.... Julio yeye ndio mshamba
Ndio ipo nchi nyingi ila haiitwi Cup Tied; Cup Tied ni kama mchezaji fulani alishacheza kwenye kombe fulani mfano FA CUP / Champions League katika msimu huo huo akihama hawezi kucheza na huko

Tukija kwenye hili suala ni mkopo / mkataba mnavyokubaliana ndivyo ilivyo sababu kama wakikataa na hio clause huchelewi kusema nipeni mchezaji wangu...

Ila hii kuna kipindi Arsene Wenger aliilalamikia..., Sababu Timu kama Chelsea enzi ina Pesa nyingi inaweza kusajili wachezaji wa kutosha na kuwakodisha kila timu..., sasa kama wachezaji hao wakiwa wanacheza na timu nyingine alafu hawachezi na Timu yako kuna unfair advantage....

Kwahio inatokea sehemu nyingi / ila sio ushamba LAKINI ikifanyika sana inaweza kuwa abused
 
Hata kama ipo ulaya na kila mahali bado inabakia kuwa ni ushamba. JE WANGEMUUZIA HATA HUKO ULAYA WANGEMZUIA KUCHEZA. huo ni ushamba na ubinafsi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…