Mtoa Taarifa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2024
- 213
- 671
Klabu ya Yanga inadaiwa kuwa katika hatua ya mwisho kumtema kocha wa timu hiyo, Miguel Gamondi na tayari imeanza mchakato wa kumnasa kocha kutoka Algeria, Kheireddine Madoui wa CS Constantine ambao ni wapinzani wa Simba katika michuano ya CAF msimu huu.
Yanga inamtaka kocha huyo aliyewahi kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika 2013-2014 akiwa na ES Setif ya Algeria na kubeba pia Caf Super Cup msimu uliofuata, wakiamini ni mdadala sahihi wa Gamondi ambaye walikuwa katika mazungumzo ya mwisho ya kila mmoja ashike lake baada ya Yanga kupoteza mechi mbili mfululizo za Ligi Kuu na sababu nyingine zinazoelezwa ni za ndani ya klabu baina ya pande hizo mbili.
Licha ya uongozi kutokuweka wazi ndoa yao na Gamondi imevunjika, mwenyewe tayari ameondoa utambulisho wa kuwa kocha mkuu wa Yanga katika akaunti zake za mitandao ya kijamii ikiwamo wa Instagram na inaelezwa anaondoshwa kutokana na vitu vingi lakini mwenendo mbaya wa timu yake kwenye mechi mbili za mwisho umetajwa kuwa sehemu ya sababu za kuondolewa.