Kocha wa Manchester United, Ralf Rangnick ameteuliwa kuwa Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Austria majukumu ambayo atayaanza baada ya kumalizika kwa msimu huu.
Pamoja na hivyo atakuwa akiendelea na mjukumu ya kuwa mshauri wa Man United jambo ambalo mashabiki wa timu hiyo wamekasirika na wamekosoa mitandaoni wakuamini hawezi kufanya kazi mbili kwa wakati mmoja.
Rangnick amesaini mkataba wa miaka miwili kuinoa Austria akichukua nafasi ya Franco Foda ambaye ameshindwa kuipeleka timu hiyo Kombe la Dunia 2022.