Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa(Taifa Stars) Charles Mkwassa abwaga manyanga

Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa(Taifa Stars) Charles Mkwassa abwaga manyanga

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,621
Reaction score
8,411
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limemteua Salum Mayanga kuwa kocha wa muda (Interim coach), wa timu ya taifa ‘Taifa Stars’.

Kocha Salum Mayanga anachukua nafasi ya Kocha Charles Boniface Mkwasa ambaye mkataba wake unafikia mwisho mwezi Machi, mwaka huu - 2017.

Kati ya majukumu yake yatakuwa ni kuandaa kikosi cha timu ya Taifa kwa ajili ya hatua ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2019 ambazo mechi za awali zitanza mapema mwaka huu.

Pia Kocha Mayanga atakuwa na jukumu la kuandaa kikosi cha wachezaji wa ndani kwa ajili ya hatua ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi ya ndani (CHAN).

TFF inamshukuru Kocha Charles Boniface Mkwasa kwa utumishi katika nafasi hiyo ulioanza Julai, 2015 na kumtakia mafanikio katika mipango yake inayofuata.

IMG_20170102_183556.png
 
Umejiuzulu au mkataba umeisha?
 
Malinzi kwanini anaandika kiingereza?

Halafu kwani by "mutual consent" manake ameacha kazi? si inaweza kuwa ameachishwa pia?
 
Atakuwa ameacha maana mkataba wake unamalizika march TFF wanazingua sana nadhani Master Mkwasa amechoshwa na ubabaishaji wa Malinzi.
 
bb178e19356305ea9cfb1d591d1d84be.jpg
Shirikisho la soka nchini (TFF) limemteua Salum Mayanga kuwa kocha wa muda (Interim Coach) wa timu ya taifa 'Taifa Stars'.

Kocha Salum Mayanga anachukua nafasi ya kocha Charles Boniface Mkwasa ambaye mkataba wake unafikia mwisho wa mwezi machi, mwaka huu - 2017.

Katika majukumu yake yatakuwa ni kuandaa kikosi cha timu ya Taifa kwa ajili ya hatua ya kufuzu kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2019 ambazo mechi za awali zitanza mapema mwaka huu.

Chanzo : Dar24
 
Tatizo la hiyo timu ni ubabaishaji wa TFF.Hawana nia ya kuandaa timu kimashindano.
 
Aende tu si tusherehekee makocha wapya maana ndo tunachoweza
 
Back
Top Bottom