Kocha mosimane aonyesha unyenyekevu licha ya kuwapatia kipigo cha kihistoria Al Ahly ya Misri katika ligi ya mabingwa ya CAF

Kocha mosimane aonyesha unyenyekevu licha ya kuwapatia kipigo cha kihistoria Al Ahly ya Misri katika ligi ya mabingwa ya CAF

Mzalendo_Mkweli

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2012
Posts
2,025
Reaction score
1,270
Yawekana Kocha wa Kibrazili Pitso Mosimane alikosekana katika mtanange uliofanyika katika uwanja wa Lucas Moripe ambapo Mamelodi Sundowns’ waliwafanyia kitu kibaya Al Ahly ya Misri kwa kuwafunga 5-0, lakini kuna mengi ya kusisimua na kujivunia jinsi huyu Mbazili alivyoshinda hiyo mechi.

Kinyume na ilivyotarajiwa, Kocha Mosimane haukuonyesha au kusema lolote la kujikuza baada walichokifanya uwanjani. Badala ya kuanza kujipia kifua na kuwaambia watu kwamba yeye na timu yake ya Sundowns ndio vidume wa Afrika kwa sasa, alibakia kuwa mnyeyekevu licha ya kwamba walikuwa wamepatia Al Ahly kipigo kikubwa kuliko vyote walikwisha vipata katika Ligi ya Mabingwa ya Caf.Ushindi huu wa kwanza wa huyu Mbrazili Mosimane ulifikiwa kwa njia ya mikakati madhubuti. Mosimane ambaye alikuwa Kocha bora wa CAF mwaka 2016 pamoja na timu yake ya ushindi (sio uchawi) waziangalia mechi Nane muhimu za Al Ahly ambapo katika hizo mechi sita zilikuwa za hatua ya makundi dhidi ya AS Vita, JS Saoura na Simba pamoja na mechi zao mbili za ligi za ligi ya misri dhidi ya Zamalek na Piramidi

"Kwanza nikiri, ni maandalizi (yaliyotusaidia kushinda mchezo huu) kwa sababu tuliangalia michezo nane ya Al Ahly," alisema Mosimane. "Tulijaribu kufinya michezo hiyo katika mawasilisho mawili ya dakika 15. Wasilisho letu la kwanza tulilifanya siku ya ijumaa (Siku moja kabla ya mechi yetu na Al Ahly) kabla ya mazoezi yetu na mwisho tulifanya wasilisho letu la pili baada ya mazoezi.Ni maandalizi yaliyotuwezesha kushinda mechi hii na sio bahati kabisa. Kilichotokea hakikutokea kwa bahati tu, aliongeza kocha Mosimane. Al Ahly labda hakujua kwamba Sundowns wanaweza kuwachimba kwa kina na kufahamu udhaifu wao kwa kiasi hiki na pia kujianda kuwakabili kwa namna ile ukizingatia kwamba sisi ni timu ndogo.

"Sidhani kwamba walitarajia hii. Lakini juu ya hayo, ni 'wachezaji wetu ambao walicheza kulingana na njia tunayocheza. Kule Misri tunaenda na tutaweka na kuongeza kasi zaidi kwa kuwatumia labda Phaka (Mahlambi), Thapelo (Morena) na Lebo (Maboe). Tutaweka kasi zaidi dhidi yao Al Ahly kwa kwa sababu watatakiwa kufunga sisi tutakapoenda kwao. Najua watajaribu kila njia kutunga goli tano.Nakuambia tunaenda kuifanya kazi yao kuwa ngumu kabisa

Sundowns tayari wameshaweka mguu mmoja katika nusu fainali za Ligi ya Mabingwa. Wao wanaenda kule pembezoni mwa mfereji wa Suez katika mchezo wao wa marudiano siku ya Jumamosi wakiwa na ujasiri kwamba mwisho mwa wiki watakuwa mojawapo ya timu nne zitakazokuwa zimesalia katika haya mashindano.Lakini kama kuna timu inayoweza kugeuza matokeo ya 5-0 basi hiyo timu ni Al Ahly ambao ni wafalme wasio na kifani katika soka la Afrika.

"Ushindi huu una maana kubwa kwa timu na watu," alisema Mosimane. "Ina maana kubwa kwangu pia.Nitasisitiza kwamba unyenyekevu ni muhimu katika kipindi hiki.


Updates
https://www.thesouthafrican.com/sundowns-cry-foul-over-al-ahly-shenanigans-after-fixture-is-moved/

https://www.sport24.co.za/Soccer/So...rules-to-destabilise-sundowns-report-20190409


Source : https://www.thenational.ae/sport/fo...-big-questions-for-egyptian-football-1.846170

https://www.iol.co.za/pretoria-news...in-the-caf-champions-leagues-history-20788088
 
Huku kwetu tulimshuhudia nahodha wa mikia fc akikosa goli tatu za wazi kabisa ikiwemo ile penati iliyoota mbawa. Kiukweli wawakilishi wetu wamejiweka ktk mazingira magumu sana.

Ukijumlisha na hizi siasa za mwamuzi walizozidandia kwa spidi ya bombadia, jibu ni jepesi tu; kufuzu hatua inayofuata ni zaidi ya mtihani.
 
Huyo kocha si raia wa Brazil ni Msouth

Sent using Jamii Forums mobile app

mamelodi kiutani wanaitwa brazilians. sabab ya jezi zao.. na jina lingine masandawana.

kuhusu mada.. mamelod ameshamfunga sana al ahly.. tena bao 3-0 ameshawai mpiga misri kule kule..

mamelodi ya miaka hii ya masimane, na tajiri yao motsepe ni kali sana.. mwaka juzi imetwaa ubingwa wa africa kwa mpira mkubwa sanaaaa. hadi waarabu wote wanaiogopa sana..
 
Huku kwetu tulimshuhudia nahodha wa mikia fc akikosa goli tatu za wazi kabisa ikiwemo ile penati iliyoota mbawa. Kiukweli wawakilishi wetu wamejiweka ktk mazingira magumu sana.

Ukijumlisha na hizi siasa za mwamuzi walizozidandia kwa spidi ya bombadia, jibu ni jepesi tu; kufuzu hatua inayofuata ni zaidi ya mtihani.
Ngoja wakapigwe goli 10 kule Lubumbash
 
Kwavile JF ni sehemu ya kujifunzia ningetazamia pia wadau wawashauri makocha au wachezaji jinsi ya behave timu zao zinaposhinda au kushindwa mechi fulani.
 
Mbona nasikia Mamelod nao wamepeleka CAF barua ya malalamiko kwa kuwa wamebadilishiwa uwanja toka Cairo na wamepelekwa kule kwenye Baridi kali. Nawashauri waendelee kuwa na unyenyekevu tu, watamulikwa tochi hadi hizo Khamsa zikamilike.
 
Huku kwetu tulimshuhudia nahodha wa mikia fc akikosa goli tatu za wazi kabisa ikiwemo ile penati iliyoota mbawa. Kiukweli wawakilishi wetu wamejiweka ktk mazingira magumu sana.

Ukijumlisha na hizi siasa za mwamuzi walizozidandia kwa spidi ya bombadia, jibu ni jepesi tu; kufuzu hatua inayofuata ni zaidi ya mtihani.
Yanga ndo watafuzu hatua inayofuata...makwasukwasu fc...ombaomba fc...gongowazi fc...vyuraaaa hahaaah....hivi huyo nahodha ndo yule juzijuzi aliyetoa pasi ya mwisho mkazamishwa kimoja cha makalioni na kagere????
 
Mazembe, Simba to battle for semifinal berth

TP Mazembe will play host to Simba SC in a Caf Champions League quarterfinal second-leg clash at Stade TP Mazembe in Lubumbashi on Saturday afternoon.

Kick-off is at 15h00 CAT (GMT +2).

The two club's played to a goalless draw in the first-leg at the National Stadium in Dar es Salaam last weekend, in a match where both teams conjured several chances to gain an advantage heading into the reverse fixture.

The woodwork came to either teams rescue throughout the match in Tanzania while John Bocco missed a second-half penalty for the hosts.

The result leaves the game in the balance heading into the second-leg in Democratic Republic of Congo, and Ravens head coach Mihayo Kazembe is mindful of the fact that a goal for Simba at Stade TP Mazembe, could make for a nervy afternoon for the hosts.

"It was a tough game for both teams. We had our chances just like them but neither of us used the minimal opportunities created," Kazembe said following the match in Dar es Salaam.

"Both teams have a chance in Lubumbashi, we will need to play with caution to make sure we don't concede a goal."

Moreover, Simba boss Patrick Aussems was pleased with the Tanzanian champions showing in the first-leg, against a side he described as one of the best on the African continent. TP Mazembe are five-time Caf Champions League winners.

"As you saw, we missed a couple of scoring chances in both halves of the game hitting the post and missing the penalty," said Aussems.

"We gave them trouble and by doing that, we have shown that we can compete with any team in Africa bearing in mind that TP Mazembe is one of the biggest club's in the continent."

The aggregate winner will face either CS Constantine (Algeria) or defending champions Esperance de Tunis (Tunisia) for a place in this year's final.

Sources : https://supersport.com/football/caf...2_Mazembe_Simba_to_battle_for_semifinal_berth

https://supersport.com/football/caf...ndowns_out_to_avoid_CAFCL_upset_in_Alexandria
 
Back
Top Bottom