Kocha mpya wa Taifa Stars, Mkwasa atangaza kikosi kipya

MeinKempf

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2013
Posts
11,093
Reaction score
7,229



KOCHA mpya wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa ametaja kikosi cha timu hiyo pia akimteua gwiji Alhaj Abdallah Athumani Seif ‘King Kibaden’ kuwa Mshauri wake wa Ufundi.

Mkwasa ameteuliwa jana kuwa kocha mpya wa timu ya taifa ya Tanzania, akirithi mikoba ya Mholanzi, Mart Nooij aliyefukuzwa mwishoni mwa wiki kufuataia kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa Uganda katika mchezo wa kwanza Raundi ya Kwanza kufuzu michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) mwakani nchini Rwanda.

Na leo Mkwasa ameteua wachezaji 26 watakaoingia kambini Jumamosi kuanza maandalizi ya kwenda kupindua kipigo cha 3-0 wiki mbili zijazo mjini Kampala, Uganda ili kusonga mbele CHAN.

Akizungumza na Waandishi wa Habari katika ukumbi wa mikutano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Ilala, Dar es Salaam, Mkwasa amesema kwamba amemteua pia Manyika Peter kuwa kocha wa makipa.

Amesema benchi lake la Ufundi linakamilishwa na Mtunza Vifaa, Hussein Swedi ‘Gaga’, Meneja Juma Mgunda na Mratibu Msafiri Mgoyi, wakati Daktari atatajwa baadaye.

Mkwasa ametaja kikosi kipya cha Taifa Stars akimtema aliyekuwa kipa namba moja chini ya Nooij, Deo Munishi ‘Dida’, akiwachukua makipa watatu; Mudathir Khamis (KMKM), Mwadini Ali (Azam FC) na Ally Mustafa ‘Barthez’ (Yanga).

Mabeki ni Shomary Kapombe (Azam), Michael Aidan (Ruvu Shooting), Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ (Simba SC), Mwinyi Hajji Mngwali (KMKM), Nadir Haroub ‘Cannavaro’ (Yanga SC), Kevin Yondan (Yanga SC), Hassan Isihaka Simba SC, Aggrey Morris (Azam FC).

Viungo ni Jonas Mkude (Simba SC), Abdi Banda (Simba SC), Salum Telelea (Yanga SC), Frank Domayo (Azam FC), Simon Msuva (Yanga SC), Said Ndemla (Simba SC), John Bocco (Azam FC), Ramadhani Singano ‘Messi’ Simba SC na Deus Kaseke (Mbeya City).

Washambuliaji ni Atupele Green (Kagera Sugar), Rashid Mandawa (Kagera Sugar), Ame Ali (Mtibwa Sugar), wakati wengine ambao wamewekwa akiba ni Juma Abdul wa Yanga SC, Mudathir Yahya wa Azam FC na Samuel Kamuntu wa JKT Ruvu.

Kesho, benchi la Ufundi la Stars litakutana na wachezaji wote walioteuliwa katika hoteli ya Tansoma, eneo la Gerezani, Dar es Salaam kuwaelimisha juu ya uzalendo na Mkwasa amesema Jumamosi timu itaenda kuweka kambi nje ya mji.
 
Apewe sapoti tu, tatizo pale TFF kuweka wazalendo tupu maslahi ya kina malinzi hayatapatikana, sasa zengwe pale litakuwa lakufikia tu, wacha tutege maskio
 
Very sad that it has taken them 10 years to realize that problems in Tanzania football will not be solved by expatriate managers. I bet Mkwasa/Kibaden alliance will go a long way.
 
Very sad that it has taken them 10 years to realize that problems in Tanzania football will not be solved by expatriate managers. I bet Mkwasa/Kibaden alliance will go a long way.

Let them try,However I am of opponent that they will not make and major differences with the same key players, same level of understanding, same level of age, same level of talents, same technical committee!

What new!

  1. Team Coach? NO
  2. Local / National Coach? No
  3. 11 fighters? No
  4. Best 22? No!
  5. Tactics and strategies from TFF? No
  6. Technical Committee? No

My opinion

  1. Invest in Primary and Secondary teams
  2. Keep on hold all regional games at CECAFA, CAF, etcand concentrate ONLY on National level games. If there are any side effects for doing this, find the best way to manage them.
  3. Start academy schools and build national team from 12 years old.
  4. Start participating on regional and internal level games in five years to come!
 
Afadhali. Kilasiku wazungu tuu! cha maana chenyewe hakionekani zaidi ya kufungwa tu. Bora hawa wamatumbi wenzetu wanaweza wakatuokoa.
 
COME BACK MAXIMO........
Bado nina imani na makocha wetu hawa, japo muda ni mdogo mno
JAMHURI aongezwe kuamsha HAMASA ya timu na kuijenga KISAIKOLOJIA....

1. UMISETA/UMISHUMTA (urejeshwe/uimarishwe)
2. Timu ziwe na A, B , WANAWAKE & KIDS
3. TAIFA CUP....irejeshwe na kuimarishwa
4. ligi za maeneo na kuchagua kombania szirejeshwe kwa kasi ya kimbunga (kijiji,kata,tarafa, wilaya, mikoa)
 
ukweli ni huu..kufukuzwa kwa MAXIMO ni moja ya makosa makubwa katika mpira wa TANZANIA.kama tungevumilia ndani ya miaka mitano au zaidi aliyosema basi naamini kwa kiwango flani tuongeona maendeleo ya mpira.lkn ndio jamaaa mume...poa tu
 

MKuu hata tukiita kocha toka mbinguni.

tatizo sio makocha tatizo ni mfumo mzima wa michezo nchini mwetu maana hata ukibadili kocha vipi unakuja kuwatumia wachezaji walewale walimfanya kocha mwingine afukuzwe kazi.

hapa inatakiwa kila wilaya angalau kuwe na academic hata 1 tuu ambayo nikubwa inakidhi mahitaji ya kiwilaya.

kuwe kunaendeshwa ligi mbali mbali za vijana na wapikwe kwa kiwango cha kimataifa disprini ni kitu mhim sana zaidi ya uwezo wa kusakata kabumbu uwanjani.

hakika tukiwa na vijana waliopikwa na kuandaliwa vilivyo kimataifa hakika automatic lazima tutatoka tuu.

ila kuendelea na hawa wavuta bangi daaa ni shida sana.

ni bora hata tukae miaka 10 tukiunda na kupika vijana kuliko kulisongesha kimagumashi na kupoteza mda
 
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania (TFF), Mwesigwa Selestine leo amemtambuisha kocha mpya wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Charles Boniface Mkwasa mbele ya waandishi wa habari.

Akiongea na waandishi wa habari, Mwesigwa amewaomba wadau wa mpira wa miguu nchini kuwapa sapoti makocha hao wazawa wanaoanza kazi kesho kujiandaa na mchezo wa marudiano dhidi ya Uganda julai 4, 2015 jijini Kampala.

Mara baada ya kutambulishwa kwa waandishi wa habari, Mkwasa amesema anashukuru kwa TFF kumpatia nafasi hiyo ya kuingoza Taifa Stars na msaidizi wake Hemed Morocco, na kuomba watanzania kuwapa sapoti.

Mkwasa amesema cha kwanza atakachokifanya na msaidizi wake Morocco ni kurudisha imani ya watanzania juu ya timu yao ya Taifa, kisha watajitahidi kadri ya uwezo wao kuhakikisha kuwa timu inafanya vizuri katika michezo inayowakabili.

Aidha Mkwasa ametangaza kikosi cha wachezaji 26 watakaoingia kambini kesho alhamisi katika hoteli ya Tansoma tayari kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa marudiano dhidi ya Uganda.

Wachezaji walioitwa ni makipa: Mudathir Khamis (KMKM), Mwadini Ally (Azam), Ally Mustafa "Barthez" (Yanga).

Walinzi: Shomari Kapombe (Azam), Michael Aidan (Ruvu Shooting), Mohamed Hussein "Tshabalala" (Simba), Haji Mwinyi (KMKM), Nadir Haroub "Cannavaro" (Yanga), Kelvin Yondani (Yanga), Hassan Isihaka (Simba), Aggrey Morris (Azam).
Viungo: Jonas Mkude (Simba), Abdi Banda (Simba), Salum Telela (Yanga), Frank Domayo (Azam).

Viungo wa pembeni: Saimon Msuva (Yanga), Said Ndemla (Simba), Deus Kaseke (Mbeya City), Ramadhan Singano "Messi" (Simba).

Washambuliaji: John Bocco (Azam), Atupele Green (Kagera Sugar), Rashid Mandawa (Kagera Sugar) na Ame Ally (Mtibwa Sugar).

Wachezaji Juma Abdul (Yanga), Mudathir Yahya (Azam) na Samwel Kamuntu (JKT Ruvu) wameitwa kama wachezaji wa akiba katika kikosi cha timu ya Taifa kinachoingia kambini kesho.

Katika hatua nyingine Mkwasa ametangaza benchi la ufundi la Taifa Stars, kocha msaidizi Hemed Morocco, kocha wa magolikipa Peter Manyika, Mshauri wa timu Abdallah Kibadeni, mtunza vifaa Hussein Swedi Gaga huku mratibu wa timu akiwa ni Alhaj Ahemd Mgoyi.

Kamati ya tiba ya TFF itapendekeza majina ya daktari wa timu na mchua misuli watakaoungana na kambi ya Taifa Stars.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
 
vyuo/ shule/ taasisi za michezo ACADEMY zianzishwe na kusimamiwa vyema,
vijana wenye vipaji na michezo husika waandaliwe na kukuzwa vyema..... NDONDI, RIADHA, NYAVU, KIKAPU, PETE , TENIS, KURUKA JUU, KURUKA CHINI, KURUSHA TUFE/SAHANI, n.k

1. BUTIMBA (KOZI YA MAKOCHA WA MICHEZO) kwa walimu waajiriwa wa serikali
2. KWIMBA (chuo cha michezo)
3. UDSM
4. MAKONGO, FILBERT BAYI, JITEGEMEE
5. KADATTA K. KADATA/ SELEMAN MATHEW (hawa wanavyuo ama timu za vipaji vya kimichezo)
6. TFF
 
Naomba watanzania wampe ushirikoano huyu kocha na wamuamini!
 
FAT (TFF).....Kwa mkoa wa DAR ES SALAAM (DRFA) ilikuwa (1990's) na timu kama SIMBA, YANGA, PILSNER, SIGARA, NYOTA NYEKUNDU ambazo zilikuwa Ligi Daraja la Kwanza (ligi kuu).
ktk mkoa huo MZIZIMA ndo ilikuwa timu ya mkoa, huku DAR STARLET ikifundishwa na makocha waliokuwa mojawapo za timu za daraja la kwanza. RASHID MAHADH, MBARAKA SELEMANI (mdogo wa MADARAKA na IDD) & HAJI MANARA, (msemaji wa Simba kwa sasa) wakiwa miongoni mwa wachezaji.
Nadhan HAJI MANARA anaweza kwa undani na uzoefu wa mchango wa DRFA katika soka la vijana na kukuza vipaji
 
Hamna kitu hapo, huyu john bocco amemuita wa nini? anaijua historia yake timu ya taifa?
 
Bwana Boniface, umeunda timu ukitaja umeweka maanani mchanganyiko. Unatafuta mchanganyiko ili kuridhisha different geographical areas au unatafuta wanaojua kucheza mpira. Nina wasiwasi usilete BRN kwenye mambo ambayo ni practical. Let us wait and see
 
Aisee hizi picha za kihindi zinaendelea ,ngoja tuone
 
John Bocco ndani tena, hivi Tanzania hatuna mshambuliaji wa kati aliye bora kupita huyu jamaa?,ngoja tuone...
 
Huenda tunahitaji molari zaidi. Ili kuweza kusonga mbele japo bado najiiza hivi hakuna wachezaji kwenye timu zote zilizoshiriki ligi zaidi ya simba na Yanga?ina maana ndanda,stand united.ruvu jkt, mgambo, costal union. Na nyinginezo wote hawana wachezaji bora wanao weza cheza taifa stars zaidi ya Simba na yanga?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…