Game ya Ajax vs Man Utd pundits walikuwa wanaiita ni boys against Men. Na ni kweli ilikuwa wavulana dhidi ya wanaume.
Edo anaweza kuwa hajawahi kucheza hata chandimu, lakini kwa mtu ambaye hajui historia yake ukimwambia hivyo hawezi kukuamini kwasababu pamoja na kutokujua amekuwa akitoa soccer consultancy nzuri sana.
Tuwe wawazi, mimi ni mshabiki wa Simba damu damu, jamaa wanaomponda sana ni mashabiki wenzangu wa Simba kwa kuwa tu kazungumzia mapungufu ya timu yetu. Ulikuwa ni ushauri tena katumia lugha nzuri sana, ila kwa kuwa sisi mashabiki akili zetu zote katushikia Manara basi imekuwa tatizo. Kwani uongo kuwa kwenye timu yetu kuna vivulana? Maana kama wangekuwa wanaume tungekuwa tulishamaliza ligi kabla ya ligi yenyewe kuisha.
Tukubali kushaurika. Waungwana ni wale ambao hukubali mapungufu yao na kuyafanyia kazi ili kuleta mafanikio zaidi. Ni kweli kuwa tuna striker wazuri, ila hatuna wauaji pale mbele. Hatuna commanding midfielder, beki yetu ya kati iko vizuri lakini ni vizuri tukianza kutafuta mtu wa kumrith maana kiukweli ukiachilia umri wa kwenye passport yake ana umri wake wa ziada.
Tukubali kushaulika kama kweli tunataka kuwa contestant wa ukweli ndani na nje ya nchi.