Kocha Mwinyi Zahera apigwa faini kwa kuvaa mavazi yasiyo nadhifu

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001
BREAKING NEWS| PAPAA ZAHERA MWINYI AKUMBANA NA ADHABU

Kamati ya Bodi ya Ligi Kuu ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi katika kikao chake cha Septemba 2, 2019 ilipitia matukio mbalimbali ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu wa 2019/2020 iliyoanza rasmi Agosti 24, 2019 na kufanya uamuzi ufatao;

Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera ametozwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa kuvaa mavazi yasiyo nadhifu na ya heshima katika mechi hiyo, kinyume na Kanuni ya 14(2m) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo. Adhabu dhidi yake imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 41(13) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Makocha.

Klabu ya Yanga imepewa Onyo Kali kwa kushindwa kuhakikisha Kocha wake Mwinyi Zahera anaongoza benchi la ufundi la timu yake akiwa katika mavazi nadhifu na ya heshima. Adhabu dhidi ya klabu hiyo ni kwa mujibu wa Kanuni ya 14(3) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.

Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amefungiwa kuiongoza timu yake katika mechi tatu za Ligi Kuu ya Vodacom kwa kutoa shutuma na kejeli kwa Bodi ya Ligi katika mkutano na waandishi wa habari baada ya mechi dhidi ya Ruvu Shooting. Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 41(9) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Makocha.

Chanzo: TFF
 
mkuu weka picha tumuone na mavazi yake ya ovyo, wengine hatuangalii mpira wa Tz kupitia televisheni.
 
Hivi hawa tifutifu wanakwama wapi mpira na mavazi wapi na wapi? Wanashindwa kusimamia soka la vijana na league kwa ujumla wanakimbilia kwenye kupigishana faini za kiduanzi kiukweli mimi ni shabiki wa Simba ila huu na uchukulia kama upuuzi wa kiwango cha lami
 
Sipendi adhabu za kuzuiwa kusema.
 
Afu eti tuna ndoto ya kucheza world cup[emoji849][emoji849][emoji849][emoji849]namna hii kweli?
 
Bengi hii sasa..
 
Wajinga sana hawa, hawataki kukosolewa. Nchi hii sasa kila mtu kaota pembe.
 
AISEEE HAWA JAMAA KWA KUIONEA YANGA..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…