OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 53,868
- 121,001
KOCHA wa Njombe Mji, Mrage Kabange anashangazwa na Yanga wanaomuita straika wa Simba, Emmanuel Okwi kuwa ni mhenga wakimaanisha umri umemtupa na amechuja.
“Wakati mwingine ni maneno ya mashabiki kama kocha ninayejua uwezo wake siwezi kuthubutu kuwaambia wachezaji wangu Okwi ni mhenga, najua anavyotumia akili nyingi za kuzifuma nyavu bila nguvu,” alisema.
Alisema aina ya uchezaji wa Okwi ni utulivu na akili, huku akiambatanisha na uzoefu wa timu mbalimbali alizozitumikia, hivyo vinamfanya awe na ufundi wa aina yake.
“Ogopa sana mchezaji ambaye anaheshimu mpira, lazima ucheze naye kwa akili kama Mbwana Samatta anapoitumikia Stars, anakuwa na soka lililoenda shule kwa kuwa amejifunza vitu vingi huko nje,” alisema.
Alizungumzia kipigo walichokipata dhidi ya Simba kuwa ni funzo kwao kuboresha uwezo wa wachezaji wao kwa mechi za mbele.